Advertise here

AKIBA NA UWEKEZAJI

FESTO AMOS

New member
*KAMA UNA NJAA YA MAFANIKIO, HILI NI MUHIMU KULIJUA*


Nilipokuwa nafundisha seminar mwezi wa 3 mwaka huu 2022 mkoani IRINGA..

Niliulizwa swali muhimu sana kuhusu swala la KUWEKA AKIBA.

Maana siku hiyo nilikuwa nimefundisha somo la hatua muhimu za kuchukua ili uweze kujenga tabia ya kuweka akiba...

Mzee mmoja mwenye BUSARA aliuliza swali kwamba,

...je tunapaswa kuweka akiba ili pesa zirundikwe BENKI badala ya kuiweka kwenye mzunguko ili uzaliane zaidi?

Hapo ndipo nilipompa majibu yafuatayo..

Nilisema kuna mambo makubwa mawili ambayo ni muhimu kuyajua..

AKIBA NA UWEKEZAJI.

Kiuhalisia wengi husema akiba ni kwa ajiri ya dharura na wengine husema akiba ni kwa ajiri ya uwekezaji..

Na wengine husema KUWEKA AKIBA NI UJINGA WA KUTOJUA KWAMBA PESA INAPUNGUA THAMANI...

Yote tisa kumi ni kweli.. Katika maelezo tunaweza kueleza tofauti na zaidi sana wengi tunafanya tofauti...

Muhimu kwako kufahamu ni kwamba..

Kuna kitu kinaitwa mfuko wa DHARURA... Huu ni mfumo ambao unashauriwa kwamba, unatakiwa uwe na pesa TASILIMU (Benk)

Ambayo inaweza kukusaidia kuishi kwa miezi 6,8 mpaka 12

Endapo ikitokea UMEFIRISIKA, UMEFUKUZWA KAZI, UMEPATA HASARA, DUKA LIMEUNGUA, BIDHAA YAKO IMESIMAMISHWA NA MAMLAKA HUSIKA, UMEUMWA, UMEFIWA, NK

Hiyo imeelezwa na wataalamu wa Kitaifa na kimataifa wa mambo ya fedha kwamba wakati unatafuta njia nyingine ya kutokea utaitumia hiyo pesa ya dharura...

Ili maisha yaweze kuendelea kama yalivyokuwa mwanzo..

Na siyo ukipata tatizo kidogo tu au usipofanya kazi kwa wiki moja tu unaanza kuwa OMBAOMBA.

Ishi leo ukiwa na uhakika na kesho yako kama binadamu mwenye utashi sahihi juu ya kesho yake..

Ukiingiza falsafa za kiimani kwamba usisumbukie ya kesho utakuwa unaangamia hivi hivi kwa kukosa maarifa, kuna wakati dharura zikitokea unaweza kusema bora usingezaliwa..

Tunaposema uhuru wa kiuchumi au wa kifedha tunamanisha...

Uwe na vyanzo vingi vya kipato, lakini pia hata likitokea janga lolote lisikufanye uwe mnyonge GHAFLA.

Pia uwe na hazina inaweza kuendesha maisha yako pale dhiki itakapotokea..

Najua unataka kuniuliza, Coach Amos vipi kuhusu UWEKEZAJI?

Safi sana... Hongera kwa swali zuri..

Hivi umewahi kusikia kitu kinachoitwa KUJILIPA MWENYEWE KWANZA? (PAY YOURSELF FIRST?)

Hii ndiyo ule mfuko maalumu kwa ajiri ya UWEKEZAJI...

Ina maana kwamba, Pesa ya akiba ni kwa ajiri ya DHARURA ndio maana wahenga walisema akiba haiozi, unatunza leo ili kije kukusaidia kesho..

(Japokuwa kuna siri nimeieleza juu ya matumizi ya pesa ya dharura ambayo msomaji wa kitabu cha mwongozo wa nidhamu ya fedha kutoka Geita ameweza kuitumia kutengeneza milioni 2 ndani ya wiki moja) alifanyaje? Pata kitabu cha Mwongozo utaona..

Ila sasa nisikilize kwa makini hapa...

Kuna mtu anasema TUNAWEKA AKIBA ILI BADAE TUWEKEZE...

Ni sahihi kabisa...

Hii hutokana na ile dhana kwamba, kila pesa usiyoitumia kwa matumizi ya kawaida wengi tunaiita AKIBA...

Ninachotaka ufahamu ni hiki hapa, bila kujali hiyo pesa unaifahamu kwa jina gani...

Ila hapo kuna kazi kubwa mbili...

Kuna ambayo inatakiwa iwepo kwa ajiri ya DHARURA (Maana hakuna aijuae kesho)

Na kuna ambayo inatakiwa kutengwa kwa LENGO MAALUMU la kiuzalishaji.

Hii haipaswi kutumika kwa sababu yoyote ile isipokuwa unaitenga huku ukiwa na malengo kwamba itakapofika kiasi fulani, utaipeleka sehemu fulani..

..Ili kuanzisha mradi mpya wa kiuzalishaji..

..Au kupanua mradi uliokuwepo ili uzidi kuzalisha zaidi..

Hiyo ndiyo maana halisi ya SAVING AND INVESTMENT.

Saving is for emergence, and Investment is for production.

Akiba ni kwa ajiri ya dharura na uwekezaji ni kwa ajiri ya uzalishaji..

Unaweza kuamua kwamba Akiba itakuwa 5% na uwekezaji utakuwa ni 10%..

Au ukafanya 10% kwa 10% yote ni mema kutegemeana na ukubwa wa kipato chako.

Nadhani kwa leo nitaishia hapo, bila shaka kuna kitu umejifunza..

Ingawa unaweza kujiongezea maarifa zaidi..

Kwa kujisomea vitabu hivi

1.NGUVU YA PESA Tsh.5000/ (softcopy)

2 Mwongozo wa nidhamu ya fedha Tsh.7000/ (softcopy)

(Wanaotaka hardcopy ni 10,000/ kwa 15,000)

Malipo yafanyike kwa mpesa 0766181367 Jina FESTO AMOS Jipimie saizi yako.

Kwa leo nitaishia hapo, niambie hapa chini kama kuna kitu umepata kuhusu akiba na uwekezaji.

BREAKING NEWS
Wiki hii, Nitakuwa nafundisha Seminar ya BIASHARA na FEDHA Kanisa la TAG Mbezi - magari saba-

Jumatano Saa 10-12 jioni
Ijumaa saa 10-12 jioni
Junapili saa 3 - 6 mchana

Kama upo Dar es salaam Unakaribishwa, hakuna kiingilio.


LIVE A GREAT LIFE

FESTO AMOS
@Coach Amos
Author | Trainer
CEO: Practical Dreamers
0766181367.


#offa #chuo #nguvuyapesa #mwongozo.
 
Back
Top