Kasomi
JT Founder
TUMA WAZO BUNIFU KUBORESHA HUDUMA ΝΑ MIFUMO YA KODI, USHINDE HADI MILIONI 50
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa fursa kwa Watanzania wabunifu kushiriki katika msimu wa pili wa kuwasilisha mawazo bunifu yatakayosaidia kuboresha huduma za kodi, kurahisisha mifumo ya utoaji huduma za TRA pamoja na kuongeza wigo wa kodi nchini.
Watanzania wanahamasishwa kuwasilisha mawazo yao kupitia tovuti ya Mamlaka katika kipengele cha Innovation, ambapo mwisho wa kutuma mawazo ni Julai 31, 2026.
Mawazo 1,000 yatakayofika kwenye Evaluation Committee yatazawadiwa shilingi 100,000 kwa kila wazo.
Kati ya hayo, washindi watakaofanikiwa katika nafasi mbalimbali watapata zawadi kama ifuatavyo: nafasi ya kwanza mshindi mmoja atazawadiwa shilingi 50,000,000, nafasi ya pili washindi wawili watazawadiwa shilingi 30,000,000 kila mmoja, nafasi ya tatu washindi wawili watazawadiwa shilingi 20,000,000 kila mmoja, na nafasi ya nne washindi 15 watazawadiwa shilingi 10,000,000 kila mmoja.
Kwa ujumla, jumla ya washindi 1,020 wanatarajiwa kunufaika na mpango huo unaolenga kuibua na kuendeleza ubunifu utakaosaidia kuboresha mfumo wa kodi nchini.
Kushiriki bonyeza hapa