Call for Interview; Kuitwa kwenye Usaili wa Ajira TRA

Kasomi

JT Founder
Dar es Salaam, 21 Machi, 2025
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza nafasi za kazi 1,596 katika fani mbalimbali
kuanzia tarehe 06 hadi 19 Februari, 2025, ambapo maombi ya kazi 135,027 yalipokelewa.
TRA imepitia kwa umakini mkubwa maombi yote yaliyopokelewa na kupata waomba kazi
112,952 waliokidhi vigezo vilivyowekwa na hivyo kustahili kuitwa kwenye usaili wa mchujo
wa kuandika (Written Interview) ambao unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29 hadi
30 Machi, 2025. Majina ya waliofanikiwa yatatangazwa kwenye tovuti ya TRA
(www.tra.go.tz) tarehe 22/03/2025 na pia taarifa itatumwa moja kwa moja kwa kila
muombaji kupitia barua pepe yake aliyotumia wakati wa kuomba kazi, Vilevile tarehe,
mahali na muda wa usaili zimeonyeshwa kwenye wito huo.

Usaili wa Mchujo wa kuandika utafanyika katika Mikoa 9 kama ifuatavyo:-
1. Dar es Salaam ambayo itahusisha waombaji kutoka Dar es Salaam na Pwani;
2. Zanzibar ambayo itahusisha waombaji kutoka Unguja na Pemba;
3. Arusha ambayo itahusisha waombaji kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga;
4. Dodoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa na
Tabora;
5. Mtwara ambayo itahusisha waombaji kutoka Mtwara, Lindi na Ruvuma;
6. Mbeya ambayo itahusisha waombaji kutoka Mbeya, Songwe na Rukwa;
7. Mwanza ambayo itahusisha waombaji kutoka Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu,
8. Kagera ambayo itahusisha waombaji kutoka Kagera na Geita; na
9. Kigoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Kigoma na Katavi.

TAARIFA KWA UMMA
USAILI WA AJIRA

Utaratibu maalumu umeandaliwa kwa waomba kazi wenye mahitaji maalumu
waliofanikiwa kuitwa kwenye usaili wa mchujo wa kuandika ili waweze kufanya usaili huo
bila usumbufu.
Mchakato huu wa ajira utaendeshwa na Mshauri Mtaalam (Consultant) na Mamlaka
itasimamia kwa karibu ili kuhakikisha haki inatendeka kwa waombaji wote. Aidha tunatoa
wito kwa waombaji kazi wote kujiandaa vyema katika hatua zote za usaili ili kufanya
vizuri katika mitihani hiyo na hatimaye kuajiriwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Waombaji watakaofaulu kwenye usaili wa mchujo wa kuandika wataitwa kwenye usaili
wa mahojiano kwa tarehe, siku na mahali watakayotaarifiwa hapo baadae.
Kwa mawasiliano zaidi:
Piga simu bure: 0800 750 075 / 0800 780 078/0800110016
WhatsApp: 0744 23 33 33
Email: huduma@tra.go.tz / services@tra.go.tz

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"
Imetolewa na:
MOSHI J. KABENGWE
Kny: KAMISHNA MKUU​
 

Attachments

  • INTERVIEW_TRA_1.pdf
    1.9 MB · Views: 377

Similar threads

Back
Top