Advertise here

Kasomi

JT Founder
FB_IMG_16485320382434668.jpg
FB_IMG_16485320317040578.jpg

pichani: Seneta Ernie Chambers


MJUE SENETA ALIYE MSHITAKI MUNGU.

Seneta Ernie Chambers, Seneta wa Nebraska Marekani mwaka 2008 alimshitaki Mungu mahakamani.

Seneta Chambers aliiomba mahakama itoe "ZUIO" la kudumu dhidi ya Mungu kufanya shughuli zake zenye madhara kama kuleta mafuriko, matetemeko ya ardhi, vimbunga, tufani na majanga mengine mengi.

Ilielezwa pia katika shauri hilo kuwa watu wengi wamekuwa wakijitambulisha kama mawakala wa Mungu na kufanya mambo mengi maovu lakini hata siku moja Mungu hajajitokeza hadharani kuwakana hivyo wanafanya yote kwa niaba yake na jina lake.

MAMLAKA YA MAHAKAMA (JURISDICTION)

Ilielezwa katika shauri hiyo kuwa Mungu yupo kila mahali ikiwemo Nebraska Marekani, hivyo mahakama za Marekani zina mamlaka ya kushughulika na kesi hiyo ya Mungu.

KUMTAARIFU MUNGU (SERVICE OF NOTICE AND SUMMONS)

Mahakama ilimtaka Seneta Chambers kuhakikisha anamtaarifu Mungu kuhusu uwepo wa shauri hilo dhidi yake mahakamani hapo kwa kumtumia nyaraka zote za kesi kupitia anuani rasmi ya Mungu ili aweze kufika mahakamani hapo kujibu madai dhidi yake. Seneta Ernie Chambers aliiambia mahakama kuwa Mungu yupo kila mahali na anajua kila kitu. Kwa kuwa Mungu anajua kila hivyo anajua pia kuhusu uwepo wa shauri dhidi yake mahakamani hapo hakuna haja ya kumtaarifu labda aamue mwenyewe kutokuja kama ilivyo kwa wadaiwa wengine.

"The court itself acknowledges the existence of God. A consequence of that acknowledgement is a recognition of God's omniscience ... Since God knows everything, God has notice of this lawsuit."

Seneta Ernie Chambers alikuwa akiita "Mungu jitokeze! Mungu jitokeze popote pale ulipo" ili ampatie nyaraka za kesi hata hivyo Mungu hakutokea.

UAMUZI WA MAHAKAMA

Kesi haiwezi kuendelea iwapo mdai hawezi kumfikia mdaiwa na kumpatia taarifa na nyaraka zote za kesi dhidi yake iliyopo mahakamani ili aweze kuhudhuria mahakamani kujibu madai dhidi yake. Mahakama imejiridhisha kuwa mdaiwa hafikiki na hana anuani rasmi hivyo ni vigumu kuserve documents zote za kesi kisheria.

Mahakama ilitupilia mbali kesi hiyo.

Seneta Chambers anasema alifungua kesi hiyo ili kukazia vifungu vya katiba ya Marekani vinavyosema milango ya mahakama ipo wazi wakati wote kwa mtu yeyote kwenye kuhitaji haki yake, pia kwamba mtu yeyote anaweza kumshitaki mtu yeyote. Kesi hii ililenga kujibu baadhi ya juhudi za serikali kutunga sheria kudiscourage baadhi ya kesi kupelekwa mahakamani
 
Back
Top