Ifahamu teknolojia ya Deepfakes, matumizi yake, faida na hasara

Kasomi

JT Founder
Ifahamu teknolojia ya Deepfakes, matumizi yake, faida na hasara.
IMG-20221224-WA0002.jpg

Teknolojia ya Deepfake inatokana na teknolojia nyingine za msingi ambazo ni machine learning (kujifunza kwa mashine) na deep learning (kujifunza kwa kina) ambapo zote hizo ni aina mojawapo za Artificial intelligence (Akili Bandia).

Deep learning algorithms ni aina ya algorithms ambazo huwa na sifa ya kujifunza zenyewe na kutafuta namna ya kutatua matatizo kwa kutumia na kuchakatua kiasi kikubwa cha data.```

So

Deepfakes technology ni6 teknolojia inayotumia mchanganyiko wa mambo ya deep learning na maudhui ya uwongo (fake contents)```

Deep ~learning~ + fake ~content~ = Deepfakes

Sasa kuna baadhi ya deep learning algorithms ambazo huwa hutumika kutengeneza contents kwenye hii Deepfakes Technology.

Kwenye hii teknolojia unaweza kufanya vitendo kama vile kubadilisha sura ya mtu A kwenye picha na video kisha kuweka picha ya mtu mwingine B.
Pia unaweza kubadilisha mpaka sauti.

Kitaalamu tunaita face swapping au face replacement.


Mfano.Unataka kumzingua Lastborn wenu sasa unaamua kujirekodi video ukawa unaigiza kama baba yenu unaanza kumfokea dogo aache utundu mara usumbufu...

Sasa unatafuta program moja ya Deepfakes unaiweka video humo kisha unaweka na picha ya baba, sura ya baba inabandikwa kwenye sura yako iliyopo kwenye video then unai-save, unamtafuta unamuonesha, mwenzio atajua kweli ni baba, kumbe unampiga mikwara tu ????.
It's funny, right?

Mara ya kwanza kuijua hii teknolojia niliiskia kutoka kwa Mteknolojia, ste kupitia kipande cha video ya music ya rapper wake pendwa Kendrick Lamar unaitwa The heart part 5 niliweza kuona Kendrick Lamar akiwa anabadilika sura mara nikaona sura ya kanye west, will Smith na wasanii wengine.

Pia baadae nikaja kugundua kuwa kwenye ile Movie ya Fast and Furious 7 ya mwaka 2017 walitumia hii teknolojia kumrudisha back to life Paulo walker ambaye aliashaga aga dunia mnamo mwaka 2013.

Teknolojia ya Deepfakes ipo na matumizi mbalimbali hutumika kwenye mambo ya
(faida - matumizi positive).

1. Kutengeneza artworks na films.
2. Kumrudisha hai mtu aliyefarika kwenye filamu au digital World (ukitumia picha ya marehemu).
4. Uelimishaji (mfano kuna video moja ya David bekham alikua anafanya kampeni ya malaria kwenye video hiyo alikuwa anaongea lugha 9.
5. Hutumika kwenye maswala biashara pamoja na matangazo
6. Hutumika kwenye video games.
7. Hutumiwa pia na baadhi ya watengeneza maudhui kwenye social media kujihusisha na watazamaji.
8. Husaidia kwenye mambo ya uchangishaji fedha na kueneza ufahamu.

Matumizi ya teknolojia ya Deepfakes.
Matumizi hasi (ya hasara).

1. Mara nyingi hutumika kwenye kutengeneza video za ngono walengwa wakiwa wanawake na watu mashuhuri.
2. Kurahisisha utapeli.
3. Kulipiza visasi - mambo ya revenge porn yaani mtu anachukua picha ya mtu yupo uchi anaweka sura yako kisha anaisambaza kama kulipiza kisasi ikiwa ulimzingua.
4. Kutengeneza maudhui ya uongo na kusambaza taarifa za uongo.
5. Hutumika kufanya unyanyasaji wa mitandaoni, kuwavunjia watu heshima.
6. Kuwatumia wanasiasa au viongozi wa dunia (marais) kueneza propaganda au kuchochea ugomvi baina ya nchi na nchi kitu ambacho hutishia amani ya dunia.
IMG-20221224-WA0001.jpg

Young will smith in Gemini Man = Deepfakes tech ilihusika

"Descrimer: haya maudhui ni kwa ajili ya uelimishaji na kujifunza hivyo basi nawaomba msitumie vibaya kuwaumiza watu wengine, mimi sitahusika".

Imeandikwa na Raven
 
Back
Top