Advertise here

Lionel Messi amekata bima ya viungo iliyo ghali zaidi duniani, ikihusisha mguu mmoja tu, wa kushoto.

Kasomi

JT Founder
BIMA YA MGUU WA KUSHOTO WA MESSI NI KUFURU
1672084012960.jpg

Lionel Messi amekata bima ya viungo iliyo ghali zaidi duniani, ikihusisha mguu mmoja tu, wa kushoto.

Mshindi huyo mara saba wa Ballon d'Or, amekata bima yenye thamani ya dola milioni 900 kwa ajili ya mguu wake mmoja tu, wa kushoto.

Kwa fedha za Tanzania, hii ni takribani trilioni 2

Wenzetu wana utaratibu wa kukata bima za viungo ambavyo wanaviona muhimu zaidi katika shughuli zao.

Kwa mfano, mcheza sinema wa Hollywood, mwanamama Bette Davis, ana bila ya pauni 400,000 ya kiuno.

Amekata bima hiyo ili kuhakikisha kiuno chake hakinenepi na kuwa kikubwa.

Mwanamuziki Mariah Carey ana bima ya dola milioni 35 ya sauti na miguu yake.

Kwa bima hii, Messi anawafunika nyota wengine wote wa michezo.

Hii ni kumi bora ya bima za viungo vya wanamichezo

1. LIONEL.MESSI - Mwanasoka
-Dola milioni 900 - Mguu wa kushoto.

2. DAVID BECKHAM - Mwanasoka mstaafu
-Miguu yote miwili na uso - Dola milioni 177

3. CRISTIANO RONALDO - Mwanasoka
-Miguu yote miwili - Dola milioni 103

4. GARETH BALE - Mwanasoka
- Miguu yote miwili - Dola milioni 100

5. VENUS WILLIAMS - mcheza tennis
- Kivundo cha mkono - dola milioni 15

6. IKER CASILLAS - Mwanasoka mstaafu (kipa)
- Mikono - Dola milioni 15.

7. FERNANDO ALONSO - dereva mbio za magari
- Kidole gumba cha mkono wa kulia - Yuro milioni 11

8. JOHNNY DAMON - Mchesa Baseball
-Macho - dola milioni 15

9. MANUEL NEUER - Mwanasoka (kipa)
- Mikono - Yuro milioni 3.90

10. MERV HUGHES - mcheza kriketi mstaafu
- Mustachi - pauni laki mbili.
 
Back
Top