Lamine Yamal akabidhiwa Mikoba ya Messi Barcelona

Kasomi

JT Founder
1752756084151.jpg

MICHEZO Rais wa klabu ya Barcelona, Joan Laporta amethibitisha kuwa winga wao Lamine Yamal atavaa jezi namba 10 kuanzia msimu wa 2025-2026 baada ya kumuongezea mkataba wa kuendelea kusalia katika klabu hiyo hadi 2031.

Yamal ambaye ametimiza umri wa miaka 18 Julai 13 2025 anarithi jezi hiyo kutoka kwa Ansu Fat ambaye ametolewa kwa mkopo kuelekea AS Monaco wiki mbili zilizopita baada ya kushindwa kuonesha kiwango bora katika kikosi hicho kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

Mhispania huyo rasmi sasa anaubeba mzigo ambao umewahi kubebwa na wakongwe waliowahi kupita katika klabu hiyo akiwepo Lionel Messi, Diego Maradona na Ronaldinho.

“Messi ametengeneza njia yake na mimi nitatengeneza ya kwangu" amesema Yamal baada ya kukabidhiwa jezi hiyo na licha ya kuwa na umri mdogo Yamal tayari ameshacheza michezo 100 ndani ya kikosi hiko huku akifunga mabao 25 na kubeba mataji lukuki ikiwemo mataji mawili ya LaLiga.

Je, unadhani Lamine Yamal ataitendea haki jezi hiyo?
 
Back
Top