TANZIA MCHEZAJI NGULI WA BRAZIL, PELE AFARIKI DUNIA

Kasomi

JT Founder
MCHEZAJI NGULI WA BRAZIL, PELE AFARIKI DUNIA
Screenshot_20221229-225438_1.jpg

Mkongwe wa soka wa Brazil Edson Arantes do Nascimento Pele amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 82 Sao Paulo Brazil baada ya kusumbuliwa na kansa kwa muda mrefu.

Pele anayetajwa kama miongoni mwa Wachezaji wa soka wa kipekee kuwahi kutokea Duniani amewahi kutwaa Kombe la Dunia mara tatu akiwa na Timu ya Taifa ya Brazil.
Nyota huyo wa zamani wa Santos FC, anayetambuliwa kama mmoja wa Wanasoka bora zaidi wakati wote, alilazwa hospitalini tangu Novemba 29, 2022 huko Sao Paulo

Ripoti ya utabibu kabla ya Krismasi ilionyesha alihitaji uangalizi kwa ajili ya ugonjwa wa Moyo na Figo, na amekuwa akipambana na Saratani ya Utumbo tangu Septemba 2021

Wakati wa uchezaji wake wa Kimataifa, alishinda Kombe la Dunia mara tatu - mnamo 1958, 1962 na 1970 huku akiwa ni mchezaji pekee aliyefanikisha hili.

Pia soma Historia ya Pele
 
Back
Top