Chukua Hii: Je, wajua kwa nini mchezaji akivua jezi uwanjani anaonyeshwa kadi ya njano?

Kasomi

JT Founder
Umewahi kujiuliza kwanini mchezaji akivua jezi uwanjani anaonyeshwa kadi ya njano? Huyu ndio mwamba aliyesababisha FIFA kukaa chini na kutunga sheria hiyo;
1742852334401.jpg

Aliyekuwa mshambuliaji hatari wa Klabu ya Manchester United Diego Forlan katika mchezo wa ligi kuu ya pale Nchini Uingereza ilikuwa ni mechi kali kati ya Manchester United na Southampton mwaka 2002, Forlan alifunga goli nzuri la kusawazisha na kisha kushangilia kwa fujo na kuvua jezi yake.

Southampton walianza mechi haraka sana na Forlan hakuwa amefanikiwa kuivaa tena jezi yake kwakuwa shambulizi lilikuwa likienda kwao alilazimika kurejea kwenye mechi haraka kuondoa mpira ambapo alifanikiwa akiwa kifua wazi.

Baada ya tukio hili, mwaka wa 2004, FIFA iliweka sheria kwamba wachezaji wanaosherehekea kwa kuvua jezi lazima wapewe kadi ya njano kama onyo.

Credit: nickymeena_
 
Back
Top