JamiiTalk Elimu; UNANIONA? HATUSEMI “ARE YOU SEEING ME?”

Kasomi

JT Founder
UNANIONA? HATUSEMI “ARE YOU SEEING ME?”

Kama kuna kitu kinawasumbua watanzania wengi ni “stative verbs”. Niliwahi kugusia kwenye moja ya post zangu, na kwenye vitabu vyetu tumeelezea kiundani sana.

Katika post hii napenda nikufahamishe kuwa HAKUNA KIINGEREZA CHA “are you seeing me?”. Kama huwa unasema hivyo basi jua ni makosa au ni Kiingereza chenu wabongo ambacho mmeamua kukianzisha na kukitumia na ndio maana mnaelewana ninyi kwa ninyi lakini mnapoongea na wazawa wa lugha yao (native speakers of English/wazungu) mnatoka patupu.

Inaweza ikatokea upo sehemu na mwenzako (mzungu), wewe unamuona lakini yeye hakuoni. Unaamua kumpigia simu na kumuuliza “Je, unaniona?”. UTASEMAJE?

Sio mzungu tu, baadhi yetu katika maeneo yetu ya kazi tunatumia Kiingereza maana ni lugha rasmi pia kulingana na sera yetu ya lugha. Inatokaea ‘situation/scenario’ kama hiyo, je utasemaje?

Nafahamu wengi wetu tukiwa katika hali hiyo huwa tunasema “Are you seeing me?”. NI MAKOSA.

BADALA YA KUSEMA “ARE YOU SEEING ME?” SEMA HIVI:
1. Do you see me? AU
2. Can you see me?

Najua utasema mbona situation iko kwenye ‘PRESENT CONTINUOUS TENSE’ lakini mimi natumia ‘SIMPLE PRESENT TENSE?’.

Ni kweli kabisa, scenario yetu ni Present Continuous Tense’, lakini verb ‘see’ katika context husika, haiwezi kutumika kwenye Present Continuous Tense. Hivyo ni LAZIMA itumike kwenye Simple Present Tense.

NAJUA HUJAELEWA CHOCHOTE, JIUNGE NA KOZI LEO KWA MAELEZO ZAIDI.

ELIMU YA BURE:
Verb ‘see’ inapotumika kumaanisha kitendo cha kuona au kuelewa, huwa ni stative verb, na HAIWEZI KUTUMIKA KWENYE PRESENT CONTINUOUS TENSE.

MIFANO:
  • I see what you mean. (SAHIHI)
  • I’m seeing what you mean. (SIO SAHIHI)
  • I see some students are not here. (SAHIHI)
  • I’m seeing some students are not here. (SIO SAHIHI).

LAKINI, inapotumika kumaanisha kitendo cha kukutana au kuonana na mtu, au kuwa na mahusiano na mtu fulani, basi inaweza kutumika kwenye Continuous tense, au mfumo wa –ing.

MIFANO:
  • I’ll be seeing teacher Wilson tomorrow.
  • They have been seeing each other for a month.
 
Back
Top