Advertise here

Maneno Matamu ya kukwambia Mpenzi wako. Achana na kuhonga hovyo utafilisika

Kasomi

JT Founder
MANENO MATAMU YA KUMWAMBIA MPENZI WAKO,,, ACHANA NA MAMBO YA KUHONGA HOVYO UTAFILISIKA✍️
1740632814217.jpg


1. “Habari ya asubuhi mpenzi wangu. Natamani ningekuwa hapo nikuamshe kwa busu tamu.”.
Anza siku yake kwa ujumbe huu mtamu utakaomfanya ahisi upendo wako hata kama mko mbali.

2. “Kila nikifikiria tabasamu lako, moyo wangu unaruka kama swala. ”.
Mkumbushe baby wako jinsi unavyofurahia kuwa naye na jinsi anavyokufanya ujihisi wakipekee.

3. “Leo nimekumbuka siku tulipokutana. Ilikuwa bahati iliyoje kukupata! ”.
Mweleze jinsi unavyothamini uhusiano wenu na jinsi ulivyobahatika kuwa naye maishani mwako.

4. “Wewe ni kama nyota angavu inayoangaza usiku wangu. ”.
Mfano huu wa kimahaba utamfanya mpenzi wako ajihisi maalum na kupendwa.

5. “Siwezi kusubiri kukuona tena. Kila dakika bila wewe ni kama mwaka. ”.
Onyesha jinsi unavyomiss na hamu yako ya kuwa naye mudawote.

6. “Wewe ndiye wimbo unaoimbwa na moyo wangu. ”.
Mfano huu wa kishairi utagusa hisia zake na kumfanya ahisi mapenzi yako ya dhati.

7. “Tabasamu lako ni kama jua linaloyeyusha barafu ya moyo wangu. ”.
Onyesha jinsi anavyokufanya uhisi furaha na joto.

8. “Asante kwa kuwa rafiki yangu wa karibu, mpenzi wangu wa dhati, na mwandani wa maisha yangu. ”
 
Back
Top