Advertise here

True story: Niliwahi kupata msala fulani nikawa nasakwa na wazee wa kazi anaandika Roma

Kasomi

JT Founder
TRUESTORY
1741508226405.jpg

Niliwahi kupata msala fulani nikawa nasakwa na wazee wa kazi 👮‍♀️ 👮

Msala niliupatia Mbeya lakini File
likatumwa Dar……Kwahiyo mbungi ikawa inachezwa Dizonga hapo kimya kimya unaambiwa kama watu wanaaga maiti!
Mi sina nijualo!!

Nina kawaida mara nyingi namba ngeni siokoti konga, labda hadi mtu aanze na intro kunitext kwanza…… Wazee 👮‍♀️ wakawa wakivuta waya siminyi cha kijani!

Kesi akakabidhiwa mwana mmoja kituo cha kati apo, mwana kasomea Cuba….. yeye akaja na strategy tofauti akaamua apite na mlango wa uwani….Akamvutia waya Stamina😁

Stamina akaokota Tambo,
Mwana akam-set Stamina yeye ni
promota anaitaka Rostam show Mwanza!😁
Stamina akajaa kwenye mfumo mamaeee
NIMEISHAAAA😁🙌🙌🙌🙌

Sema tu Stamina hakuwa na machale, maana naskia jamaa hela aliyotajiwa alikubali fasta sana, hakunaga promota wa hivo bana lazima bargaining i-take time kidogo mvutane!!

Na chakushangaza jamaa akamwambia Stamina nataka kulipa leo leo nigeuze Mwanza nikaanze maandalizi ya show😁

Lakini lazima muwepo nyote na Roma kuna mkataba lazima msign wote pamoja!!

Back to me….. Mimi jana yake nilikuwa vitu sana, kwahiyo nimezima mwili hadi simu, Stamina hanipati, akampigia Mama Ivan.

🗣️Oyaaa muamshe mumeo anapishana na gari la Bank, mwambie awashe simu fastaa kuna mchongo!!

Mluguru ana njaa sana yule angejua kumbe anaenda kunitia kiberiti!!

ITAENDELEA

✍️Roma Mkatoliki

Toa maoni yako
 
TRUE STORY 2
1741508356400.jpg

Inaendelea.....

Mluguru ana njaa sana yule angejua kumbe anaenda kunitia kiberiti!!

Mimi baada ya kuamshwa, 📞 enhee maelekezo ka’mkubwa…..!?

🗣️Oyaa ibuka Sinza wanyama hotel sita kamili tufunge kipindi, Rostam Mwanza Jumamosi ijayo jamaa anatoa Milio kadhaa (Dogo aka-name the price) Mmh nikaguna!!

Nways mimi nilimuitikia lakini nikasema sitaenda eneo la tukio mpaka wao kwanza wafike then nipime ni deal kweli au manjegeka!

Sita na nusu naskiaa ngrrrr ngrrr……
📱 oyaaa hufiki? Niko na mwana hapa unasubiriwa wewe tu, mwisho jamaa waghairi wakawape mchongo Weusi😁

Sema kwenye haya maisha bana amini sana Instinct zako, moyo wangu ulikuwa mzito sana kwenda!

Stamina alikuwa na mchizi wetu mwingine wameenda naye, nikamwambia hebu mpe tambo huyo mchizi wetu niseme naye!!

Mimi sasa 🗣️📞 oyaa Arbabu mambo vipi? Huyo mwana ukimzoom ni promota kweli au geti jeusi?

Mwanetu akawa half half, akanipa aaah inawezekana, kwani una msala wowote? sema ana begi hapa anaonekana anatoa hela huyu….we roho yako inakuambiaje?😁
Arbabu ananiuliza mimi tena jamani😁

Nways nikaona liwalo na liwe sijaua sijahujumu uchumi, yatazungumzika!! Nikawasha pira hadi sinza….. Nikapark pira sehemu nikaitisha bajaji hadi eneo la tukio.

Nikamwambia bajaji usizime chombo halafu kaa mkao wa mwendo wa ngiri kinyeo juu….kuwa hewani!!

Sasa unajua sio Stamina wala yule mchizi wetu aliyekuwa anajua kama mimi nina msala nawindwa!!

Nilipomuona yule promota
kuna ka-inner sound kakanambia amshaa…. kuna sauti ingine ikanambia sikilizia mchongo!!

Always trust your first sound!!
Mimi sikutii haya mamlaka!!
Kosa kubwa sana nilifanya!!

✍️Roma Mkatoliki

ITAENDELEA...
 
TRUE STORY 3
1741508226405.jpg

Inaendelea...

Sasa unajua sio Stamina wala yule mchizi wetu aliyekuwa anajua kama mimi nina msala nawindwa!!

Nilipomuona yule promota
kuna ka-inner sound kakanambia amshaa…. kuna sauti ingine ikanambia sikilizia mchongo!!

Always trust your first sound!!
Mimi sikutii haya mamlaka!!
Kosa kubwa sana nilifanya!!

Mezani maongezi yakaanza,nikamuuliza ni show ya nini akajibu ya uzinduzi wa hotel ya tajiri fulani Mwanza✅

Alipojichanganya mchizi ni nilipomuuliza inaitwaje hiyo hotel?😁

HE DIDN'T SEE IT COMING😁

Kwanza aka-take time kujibu, then akataja jina hilo Hakyamungu sijawahi kulisikia sio tu Mwanza, Kanda ya ziwa yote😁

Nikaona hii “RED FLAG”

Sasa mchizi (Promota) kwanza kila saa ana jisachi kwenye begi lake anachokitoa hata hakionekani!!
anazuga kama anatoa makaratasi hivi anadai ndio mkataba tusaini, mara tena anaurudisha kwenye begi, anazuga tena busy anaongea na simu na mtu anamuita afike pale!

Akatuambia mtu wake inabidi aje naye hapa kuna na sign yake ashuhudie…..anafika sasa hivi tumskilizie!!

Aaaah usintanie weweee machale kundesa…..Nikaona hii KASONGO TAYARI mbona wewooo!!

nikazuga zile za kupiga 100 (Customer Service) halafu najidai kama naongea na mtu niko around……😁 Mpaka kwenye Bajangwe 🛺 langu,
Amsha Babaaa Amshaaaa…..Amshaaaa😁😁 Nduki moja nene Tuisila Kisinda Forward ya boli!!

Dakika 3 tu mbele natumiwa msg na mwanetu yulee arbabu nilieongea naye….ananambia usigeuke kala sepaaaa msalaaa!!

Moyoni nikajisemea una masikhara wewe mi niko njia ya clouds huku cocacola now naitafuta mbezi ya chini😁

Kumbe pale wanyama hotel jamaa ndio alikuwa anawasiliana na wenzake, so zikadondoka Njagu kama sita hivi……🙌🙌🙌🙌🙌

Mwana akawambia Mkato kasepa sasahivi!!

OYAAAA HAPO NISHAFIKA KWA ZENA KULE 😁

Nyieeeee 😁🙌🙌🙌🙌🙌

Jioni nikapokea Text…..

TUMEKUKOSA LEO LAKINI TUTAKUDAKA TU!!

✍️Roma Mkatoliki

ITAENDELEA....
 
TRUE STORY 4

Inaendelea...

Jioni nikapokea Text…..

TUMEKUKOSA LEO LAKINI TUTAKUDAKA TU!!

Aaah nikaona huu mchongo umeshakuwa serious sasa!! Nikatupa taulo 🙌🙌🙌

Kesho yake asubuhi sana I DECIDED TO TURN MY SELF IN!!

Nikajipeleka kituoni mwenyewe tukayazungumza na nikaadhibiwa….na waliniTreat vema sana Mungu ampe maisha marefu mkuu yule wa kituo
(Police Wema Bado Bado Wapo)

Funny part….😁😁 Yule Askari aliyepewa file akajifanya promota…..akaambiwa nipo pale kituoni akaibuka akanikuta,
kwanza tulipotazamana wote tukacheka saanaaaa😁😁😁

Kitu cha kwanza akanambia

Ujue Mkato pale uliponiuliza Jina la hotel ndo’ uliponivuruga pale…..😁 Sijui hata nilitaja jina gani nilijisemea tu!😁

Khaaa Lile jina kwakeli silikumbuki ila halisound kabisa kihotel, tena ya tajiri!! 😁

Nikatumikia adhabu, tukabadilishana namba na Promota wangu 😁 Mpaka kesho tumekuwa wana sana na ni shabiki mkubwa wa muziki wangu!!

MAISHA YANA SIMULIZI NYINGI SANA!!

Ikapita wiki moja hivi Stamina akanipigia simu akanambia!!

Kaka kuna jamaa wa Mbeya wanata Show!!

Nikaguna Mmh…Tuliishia kucheka sana mpaka simu ikakatika!!😁

ANYWAY.......GET READY ROSTAM NEW PROJECT

AFTER RAMADHAN 🤲🏆

MWISHO..!

Stay turned kwa story nyingine mpya

✍️Roma Mkatoliki
 
Back
Top