Advertise here

Mchungaji aliyetekwa aeleza mateso na kwenda kutupwa porini ashindwa kutembea "Mengine tuyaache "

Kasomi

JT Founder
Mchungaji aliyetekwa aeleza mateso na kwenda kutupwa porini ashindwa kutembea "Mengine tuyaache "
Screenshot_20250517-173414~2.png

Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Kristo lililopo Mtaa wa FFU, Kata ya Murieti, Steven Jacob Gumbo (35) ambaye iliripotiwa ametekwa na ‘Watu Wasiojulikana’ Mei 16, 2025 amezungumza na Wanahabri na kueleza kuwa Watu waliomchukua walijitambulisha kuwa ni Askari Polisi na wanamhitaji kwa ajili ya mahojiano

Amesema Watu hao walimchukua kwa nguvu huku wakimpiga, akapelekwa sehemu ambayo hakuifahamu na kuingizwa kwenye chumba kisha kuanza kumshambulia

Ameongeza “Naomba nisiongee mengi, sababu ya kutekwa ni ishu za Mtandao. Walichukua maelezo, wakanipeleka porini West Kilimanjaro, wakachukua simu yangu na kunitaka nifute video zangu zote, wakazungumza vitu ambavyo siwezi kuvisema kwa sasa kisha wakanitelekeza hapo.”

Awali Taarifa ya kupotea ilieleza Hivi

"Mchungaji wa kanisa Huduma ya Kristo lililopo mtaa wa FFU kata ya Murieti Jiji Arusha Steven Jacob mwenye umri wa mika 35 alitekwa na watu wasiojulikana asubuhi ya Tarehe 16 May 2025 wakati akitoka nyumbani kwake

Wakizungumza mashuhuda na majirani wa eneo hiyo akiwemo baba yake mzazi ambaye ni balozi wa CCM katika shina hilo wamesema waliomteka walifika na gari aina ya Land Cruser lisilokua na namba za usajili ambapo walimkokota kwa nguvu huku mchungaji huyo akipiga kelele za kutekwa lakini haikusaidia na walimtupa kwenye gari kisha kuondoka nae"

CHANZO: KUSAGA TV
 
Mchungaji aliyetekwa aeleza mateso na kwenda kutupwa porini ashindwa kutembea "Mengine tuyaache "
View attachment 1102

Alitekwa na vijana wa ccm maarufu CHINJACHINJA amshukuru Mungu baba yake ni balozi wa ccm wangemuua na kumtupa.
 
Back
Top