Kasomi
JT Founder
Mwaka 1995 aliyewahi kuwa Muumini wa katoliki Joseph Kibweteere wa Uganda Alitangaza Kuwa Mwaka 2000 Ndio Mwisho wa Dunia, Hivyo Kanisa Lake Linauza Vyeti Kama Ndiyo Ticket ya Kuingia Mbinguni. Siku Ilipofika Watu Walijaa Kanisani, Akafunga Milango na Madirisha Kisha Akatia Kiberiti Kanisa Zima. Watu 778 Walikufa.
Tukio linaanzia mwaka 1989 ambapo Muumini wa kanisa katoliki mjini Kanungu Uganda Joseph Kibweteere alifuatwa na mwanamke Credonia Mwerinde, kahaba ambaye alidai kuwa alikuwa akitaka kutubu dhambi zake huku akisema ikiwa atampokea basi ataiona sura ya bikira maria, kwani yeye alikuwa ameoteshwa hivyo ndio maana akamfuata.
Ni kweli Joseph alimpokea mwanamke huyo na siku chache baadae akadai alikuwa ametokewa na bikra maria.
Siku chache baadae Kibweteere na viongozi wengine wachache wa Kikatoliki wakaamua kujitenga na kanisa katoliki na kuanzisha kanisa lao la miujiza. Viongozi waliounda kanisa hilo walikuwa ni Ursula Komuhangi, Credonia Mwerinde, Joseph Kibwetere na Dominic Kataribabo (wote bado wako hai).
Kanisa lao waliliita 'Urejeo wa amri kumi za Mungu' ambapo lilijizolea umati wa waamini mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Mwaka 1995 Joseph Kibweteere ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa kanisa hilo alitangaza kwamba mwisho wa dunia utakuwa mwaka 2000. Alitangaza kwamba kanisa lake lingetoa msamaha wa watu wote watakaonunua sukuk ili kuingia mbinguni.
Ilitangazwa kuwa kila mmoja anaetaka kuingia mbinguni baada ya mwisho huo wa dunia walioutangaza kuwa ni mwaka 2000, alikuwa anatakiwa kununua sukuk kanisani hapo ikiwa ni 'kuweka hazina yake mbinguni'. Ulitakiwa kulipia fedha nyingi kisha unapewa Sukuk ambayo ndio kibali chako cha kuingia mbinguni.
Sukuk hiyo ilikuwa ni kama Deed au Certificate fulani unayopewa ya kuonyesha ni kweli umekidhi vigezo na umekua veryfied kuingia mbinguni.
Watu walianza kuuza mali zao ili wapate fedha za kulipa ili wapatiwe sukuk ya kuingia nayo mbinguni, lakini pamoja na ujio wa mwaka wa 2000, hakuna kilichotokea hivyo kuibua mashaka na hasira kwa wakazi ambao walikuwa wamepoteza kila kitu kwa ajili ya kununua sukuk hizo kwa bei kubwa.
Kibweteere alituliza mashaka ya watu hawa na akatangaza kwamba tarehe 17 Machi ya mwaka 2000 ndiyo itakuwa rasmi mwisho wa dunia, na kwa tukio hili aliamua kufanya karamu kubwa aliyoiita “Karamu ya Mwisho” kusherehekea kuingia mbinguni.
Siku ilipofika aliwaita wale wote walionunua hati za kuingilia mbinguni, Watawa waliandaa chakula na kila mmoja alikula na kunywa kisha milango ya kanisa ikafungwa. Joseph akaanza kuwaua baadhi yao na kuwashawishi wengine kujiua wenyewe ili kuwapeleka mbinguni.
Baadaye usiku inaelezwa kuwa viongozi hao wakiongoza na Joseph Kibweteere walichoma moto kanisa zima na kusababisha waumini 778 kufariki ndani humo akiwemo yeye mwenyewe.
Ingawa Joseph na wenzake walidhaniwa kuwa walikufa katika tukio hilo, polisi wa Uganda mwezi mmoja baadaye walitoa taarifa ya kuwa walikuwa wamewakamata viongozi wengine wa kundi hilo. Mwaka 2014 taarifa ilitangazwa na Polisi wa Uganda kwamba kulikuwa na ripoti kwamba Kibweteere alikuwa amejificha nchini Malawi.
Hakuna taarifa inayoeleza nini kilitokea kwa viongozi hao, lakini ni kwamba Joseph Kibweteere yuko hai mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 91, na hata Credonia Mwerinde yuko hai pia akiwa na miaka 71.
Japo Serikali ya Uganda ilisema kuna uwezekano alikufa pamoja na wafuasi wake, lakini pia haikupata uthibitisho wa mwili wake. Wengine wanaamini alikimbia na huenda aliendelea kuishi kwa kujificha.
Kwa hiyo, kibwetere anahesabiwa kama mtu aliyepotea, na hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuthibitisha kifo chake.