Advertise here

PENZI LA JESCA

Euro Man

New member
CHOMBEZO: ""PENZI LA JESCA""
SEHEMU YA KWANZA
MTUNZI: ENOCH LIBERATUS.

WHATSAPP NO:0622724691.

Alikuwepo jamaa mmoja ambaye kwa jina aliitwa Mr Abby jamaa huyo alikuwa na mpenzi wake ambaye alimpenda sana jina lake aliitwa Jesca,mapenzi yao yaliweza kudumu kwa muda mrefu zaidi toka walipokuwa wakisoma shule ya sekondari, wapenzi hao walikuwa wakiishi katika jiji la Arusha ,wote walikuwa wakisoma sekondari katika shule moja na walipo hitimu Elimu yao ya sekondari, Mungu si Athumani wote walifanikiwa kufaulu masomo yao yaliyoweza kuwaruhusu kuendelea hatua nyingine ya elimu.

Mr Abby alifanikiwa kwenda chuo moja kwa moja alienda kusoma chuo cha Ualimu kilichokuwa kinapatikana Mwanza ila kwa upande wa Jesca yeye alifanikiwa kwenda kidato cha tano nakumalizia kidato cha sita mkoani Tabora,baada ya kumaliza kidato cha sita alifanikiwa kwenda chuo kikuu UDSM kilichopo Jijini Dar es salaam

Ingawa kila mmoja alikuwa mbali na mwenzake ila walizidi kupendana na kuwasiliana mara kwa mara pale walipo pata muda, Baada ya miaka mitatu Mr Abby aliweza kuhitimu masomo yake ya chuo kwasababu yeye alikuwa amesomea diploma ya ualimu,na alipomaliza chuo alirudi nyumbani kwao Arusha huku akisubiri kuajiriwa na Serikali, Baada ya miezi Saba mbele Mr Abby alifanikiwa kuajiliwa katika shule ya serikali iliyokuwa ikipatikana jiji la Mwanza ,huku kwa upande wa Jesca yeye alikuwa bado akiendelea na masomo yake.

Jesca alikuwa Mwanamke mzuri sana ambaye alikuwa na kila sifa zenye kumvutia mwanaume ambaye siyo rijali,Jesca Mungu alimjalia sura nzuri na ngozi yake ilikuwa yenye rangi nyeupe na yakuvutia amabayo ilikuwa kivutio kikubwa sana kwa wanaume wengi, pia Jesca alikuwa na umbo matata shepu namba 8 na macho mazuri ya kulembua , kila mwanaume aliyemtazama alivutiwa nae kutokana na uzuri aliokuwa nao kwani avae dela au gauni nyuma palijichora umbo namba 8,msambwanda wake kila alipopita wanaume wengi walikuwa wakigeuza shingo zao nyuma ili kuungalia kwakuwa ulikuwa ukitetema kama tetemeko la ardhi.

Mizizi ya mapenzi kati Jesca na Mr Abby iliendelea kukuwa zaidi bila kujali umbali waliokuwa nao , mapenzi yao yalikuwa mazuri sana tena kwakuwa Mr Abby alikuwa amesha mtambulisha mchumba wake kwa wazazi wake vivyo hivyo kwa upande wa Jesca alikuwa amekwisha mtambulisha mpenzi wake huyo kwa wazazi wake,huku wote wakiweza kuahidiana ahadi kemu kemu kuwa wangeweza kufunga ndoa mara baada ya Jesca kuhitimu masomo yake ya chuo kikuu .

Jesca aliendelea kufanya vizuri katika masomo yake hatimae alifika mwaka wa mwisho wa masomo yake ikiwa ni mwaka wa tatu akiwa hapo chuoni,katika kipindi chote Jesca alipokuwa hapo chuoni aliweza kusumbuliwa na vijana wengi wakiwemo Walimu na wanachuo wenzake ila kati ya wote waliomsumbua hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kulipata penzi la Jesca wanaume wengi walimtamani kimapenzi, na baadhi yao walidiliki kumlazimisha Jesca ila aweze kuwakubalia kwa kuweza kuwa nao katika mahusiano huku wengine wakimuahidi kuwa wangeweza kumuhudumia na kumpa kila kitu atakachokihitaji ,wengine wakidiliki kumlazimisha Jesca Kufanya mapenzi hata kabla hawajakubaliwa,""uzuri wa Jesca uliwachanganya wanaume wengi chuoni hapo""

Wanaume wote walio msumbua Jesca hakuna mwanaume hata mmoja aliyepata bahati ya kuwa na Jesca katika mahusiano ya kimapenzi kila Mwanaume aliyemfata Jesca ,Jesca hakuwa mtu wa kuuficha ukweli alikuwa akiwaambia kuwa anampenzi wake tayari na anampenda sana,hivyo hawezi kumsaliti kwa kutoka kimapenzi na mwanaume mwingine kwakuwa alikuwa na upendo wa dhati kwa Mr Abby.

Ilikuwa ni mwanzo mwa mwaka ikiwa ni mwezi wa pili mwaka 2018 Jesca kuwepo hapo chuoni ,mwaka huo ulikuwa ni mwaka ulioambatana na misukosuko na majaribu mengi kwa upande wa Jesca ,Mkuu wa chuo aliyeitwa Amoni Saimon aliweza kumleta Mwalimu mpya katika chuo hicho ambapo aliweza kumtambulisha Mwalimu huyo mbele ya wanachuo wote ili waweze kumfahamu,wanachuo wote waliitwa ili kuweza kumpokea Mwalimu huyo.

Mkuu wa chuo Amoni Saimon aliweza kumkaribisha Mwalimu huyo mgeni ili aweze kujitambulisha mbele ya wanachuo wote ,Mwalimu huyo alisimama na kuanza kujitambulisha kwanza aliwasalimia kisha akasema""Mimi naitwa Mwalimu John Charles,ninatokea Singida ila ninaishi hapa Dar es salaam nitakuwa pamoja nanyi kwa muda wote nitakao kuwa hapa,nacho hitaji kutoka kwenu ni ushirikiano Asanteni '" baada ya Utambulisho huo wanachuo wote walimpigia makofi kama ishara ya kumkaribisha .

Mwalimu Charles alikuwa mrefu na mwenye mwili wa wastani,kwa kumuangalia tu alionekana mtu aliyekuwa akijipenda sana,siku alikuwa amevalia,T-shirt,suruali aina ya kadeti na raba nyeupe,mwalimu huyo alikuwa mzuri kweli kwa sura,kwa kumuangalia alionekana bado kijana mdogo sana hiyo ni kutokana na jinsi alivyokuwa akijipenda na mwili aliokuwa nao wa wastani,baada ya Mwalimu John Charles kujitambulisha aliwashukuru kwa ukaribisho wao kisha wanachuo wote wakawa wametawanyika kuendelea na majukumu yao.

Ujio wa Mwalimu John Charles katika chuo hicho ndio ulikuwa mwanzo na chanzo cha Jesca kuishi maisha magumu kwasababu Mwalimu John alikuwa akimsumbua sana ,kwakuwa baada ya kufika hapo chuoni alitokea kumpenda sana mtoto mzuri Jesca, hivyo alijaribu kutumia kila mbinu ili kuweza kumteka kimapenzi , bila kujali ni mara ngapi amemfata Jesca kumtongoza na kukataliwa ila kwakuwa Mwalimu John alikuwa ameshadata kwake hakuwa tayari kumkosa kizembe.

Jesca alijitahidi kumwambia ukweli kuwa ""yeye ana mpenzi wake ambaye anampenda sana kupita kiasi na hawezi kumsaliti"" ila kwa maneno Jesca aliyokuwa akimwambia Mwalimu John,hayakuweza kusaidia kitu na hayakuweza kumzuia Mwalimu John kuendelea kumfuatilia.

ITAENDELEA.....
 
Wow ????????????
 
Back
Top