Advertise here

Maswali mawili niliyoulizwa sana

Minga

New member
Leo naomba nitoe majibu ya haya maswali mawili;
1::Naamua nisimtafute lakini najikuta namtafuta tena.
2::Ananifanyia mabaya lakini nashindwa kumuacha.

Changamoto inayosumbua hapa ni ufahamu na sio upendo.

Wengi wanazani wanashindwa kwa sababu et wamependa... Hapana! ila shida ni kwamba hawajui upendo ni nini.

Wengi hawajui kwamba kinachowaendesha hapo ni hofu ya upweke, hofu ya kujitegemea na mazoea.

Na upendo ulishakufa zamani sana. Tuone namna ya kutoka hapo sasa;

Unapaswa ujifahamu vya kutosha.

Kujijua ni kuona thamani yako nje ya mtu mwingine.

Kama hujajijua, utajiona kama mtu mwenye kasoro, bila yeye unajiona haujitoshelezi kwa sababu haujijui, laiti ungejijua na kuelewa thamani yako usingekubali kujipoteza wewe kwa ajili ya mtu asiyejali uwepo wako.

Mbili, Unaogopa pweke.

Upweke umekuumbia sauti ya uongo ndani yako inayosema, "Ni bora kuwa na mtu anayekuumiza kuliko kuwa peke yako"

Nawewe umekubali.🤔

Ukweli ni kwamba mtu anayekuumiza ni hatari kuliko upweke.
Upweke sio gereza ila ni wakati unaokukumbusha unapaswa kujigundua zaidi...unapaswa jitafute hadi ujipate

Kitu cha tatu: Umeweka agano la damu.

Mara nyingi ni ngumu sana kumsahau au kuachana na mtu aliyekufungua kwa mara ya kwanza.

Kuna kuwaga na mvutano mkubwa sana hapa, kwa sababu hii si juu ya tendo tu ila ni muunganiko wa nafsi, wewe na yeye mmekuwa kitu kimoja, suruhu ni kuivunja hiyo bond.

So wakati mwingine unaweza kuwa na mahusiano yanayovunjika na yasiyofanikiwa huwenda shida ni hiyo kwamba bado wewe ni mtu wa yule mtu aliyekufungua.

4::Unapaswa uufahamu upendo wa kweli na namna ya kuupata.

Wengi wetu hatujui chochote kuhusu upendo hivyo tunavumilia mahali panapotumaliza kabisa.

5::Unataka kumbadilisha.

Huwezi kumbadilisha mtu ambaye hajaamua kubadilika.

Lakini wengi tunajitumainisha kwamba mtu huyo atabadilika siku moja.

Ndio maana unavumilia mahali ambapo hapakupaswa kuvumilia na mwisho wa siku utajikuta ulikuwa unapoteza muda na utajiraumu kwa uzembe wako.

6::Ikumbuke thamani yako uliyoisahau.

Sio kwamba unampenda huyo unayemng'ang'ania isipokuwa umesahau kwamba hata wewe ni wa thamani pia kwako.

Ukikumbuka kwamba na wewe ni wa maana utajua kwamba kumuachilia huyo mtu ni heshima na faida kuliko kuendelea kushikilia hilo kaa la moto.

7:: Rejesha nafasi ya Mungu mahala pale.

Wakumng'ang'ania ni Mungu, badala ya kuhangaika na huyo mtu wekeza muda kumwabudu Mungu, huko kuna faraja ya kipekee utakutana nayo.

Kwakadri unavyomtafuta Mungu ndivyo utakavyokuwa unajipata wewe.

Mungu ndiye hatima ya maisha yako na sio mtu.

E.M✍️
 
Back
Top