Advertise here

Fahamu kuhusu ChatGPT Artificial Intelligence Tool inayoweza kufanya maswali na kuchat

Kasomi

JT Founder
Fahamu kuhusu ChatGPT Artificial Intelligence Tool inayoweza kufanya maswali na kuchat

ChatGPT ni Artificial Intelligence tool iliyo anzishwa mwishoni mwa mwaka 2022 na kampuni la OpenAI.
Umeshajiuliza hii Tool inafanyeje kazi?
Ngoja kasomi nipuke hii kidogo

Watu tushazoea ku Google kama tuna swali ili kujua majibu, sasa Google ukisearch unaletewa links kibao kisha unachagua wapi usome ili kupata jibu...

Achana na Google hii Artificial intelligence tool yenyewe inakupa majibu ndani ya seconds tu hamna mambo ya link link yenyewe inacharaza tu maandishi shwaaa ishamaliza.

Tool hii ukiitumia vizuri inaweza kukusaidia kwenye shughuli zako za kila siku kama kukusaidia:
1. Kufanya assignment au homework
2. Kufanya research.
3. Kuelewa na Kusolve maswali magumu mf. Math, chemistry, physics etc
4. Kuandika Essays, Articles, Barua, CV, Poems, Report e.t.c
5. Kupata content ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii.
6. Kupata project ideas.
7. Kuandika misimbo coding, kufanya debugging etc.
8. Au Unaweza chat nayo mkapiga story, Kukuambia matani au kukupa ushauri.

Yes, Hayo yote ni kweli na yanawezekana.

Hii tool itakusaidia KUOKOA MUDA na kufanya MAMBO YAKO KWA UHARAKA ZAIDI na kuongeza UZALISHAJI/ PRODUCTIVITY.
Itakusaidia kuongeza MAARIFA na kungeza UFAULU chuoni.

Binafsi sikuwa mchoyo kwa Wadau wangu wa JamiiTalk kuwashirikisha hilo.

Sasa kituu pekee kinacho fanya ChatGPT iwe nzuri kwa watumiaji hata uulizaji wake wa maswali unaweza uliza kama unaongea na Mdau wako tu.
Kwa mfano unaweza uliza swali kishikaji kama hapo chini, na yenyewe itakujibu kishikaji hivyo hivyo.
1674594042996.jpg

Baada ya kuona Artificial Intelligence Tool hii ipo nikakumbuka JamiiTalk tukianzisha jukwaa la Jamii Ask (Q & A) ambapo tulimtambulisha na FatherBot jukwaani hapo kwa ajili ya kusaidia Majibu, sasa tutajitahidi pia na sisi FatherBot kujibu maswali Yenu endapo mukiuliza na kumtag kwenye hilo jukwaa.

Jinsi ya kujisajili na ChatGPT
Kujisajili Tembelea tovuti ya OpenAI kisha juu kuna alama ya ChatGPT bonyeza hapo au unaweza bonyeza hapa www.chat.openai.com kisha tengeneza account kwa kujaza email au unaweza sign with Google account au Microsoft account baada ya hapo utaweka namba za simu kisha utatumiwa verification code.

Ingiza hizo code hapo utakuwa umefungua account ya ChatGPT na utauliza.

Kama hujaelewa au kukwama acha comment yako tutarejea kwa ajili Yako.

1674593908144.jpg

Tool hii unaweza kuuliza kwa kiswahili ila yenyewe itajibu kwa kingereza
 
Back
Top