Maduka yavunjwa Mkoani Geita katika mtaa wa Mbugani Kata ya Kalangalala Bidhaa zaibiwa

Kasomi

JT Founder
Maduka yavunjwa Mkoani Geita katika mtaa wa Mbugani Kata ya Kalangalala Bidhaa zaibiwa
Screenshot_20250516-154702~2.png

Maduka manne ya wafanyabiashara katika mtaa wa Mbugani Kata ya Kalangalala katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita yamevunjwa na bidhaa zilizokuwemo ndani kuibwa.

Wakizungumza na EastAfricaTV wafanyabiashara walioibiwa bidhaa zao wamesema majira ya saa 10:00 usiku walipata taarifa juu ya wizi huo ambapo walianza jitihada za kumtafuta Mkurugenzi wa kampuni ambayo ilikuwa ikilinda eneo hilo.

Msimamizi wa kampuni inayohusika na ulinzi eneo hilo James Kitulo amekiri wizi kufanyika katika lindo lake ambapo amesema jitihada zinaendelea za kuwatafuta walinzi ambao walikuwa zamu huku akiahindi kulipa gharama zote.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mbugani Jumanne Bayasabe amemshikilia msimamizi huyo ili aweze kutoa ushirikianao ikiwemo kufahamu waliokuwa zamu huku Afisa Mtendaji wa kata ya Kalangalala Hamad Hussen amethibitisha kutokea kwa tukio na kuitaka kampuni hiyo kutenda haki ikiwemo wafanyabiashara kulipwa fidia zao.
 
Back
Top