Advertise here

Faida Potea atangaza kugombea Ubunge jimbo la Nyamagana wilayani mwanza

Mtata

Member
Screenshot_20250518-172200~2.png

Natangaza kugombea ubunge jimbo la Nyamagana wilayani mwanza..

Wanabodi amani iwe nanyi na poleni na majukumu ya kutafuta rizki....

Jimbo la nyamagana ni jimbo lenye heka heka nyingi sanaa za kisiasa, ni kiini cha mabadiliko katika nchi hii, ni kati ya maeneo yenye historia kwenye medani za kisiasa,, jimbo hili liko chini ya CCM toka litoke mikononi mwa Chadema Mh Weche, nimeamua kujitosa kugombea jimbo la nyamagana kupitia chama changu CCM,, sifa zote ninazo, nitafuata taratibu zote ndani ya chama changu ,,nitayasikiliza na kuyahishimu mawazo na maoni ya viongozi wangu wa chama,, umri wangu unaniruhusu,jimbo lile kwa sasa linahitaji mtu ambaye ataweza kuendana na pilika pilika za maendeleo ya haraka kwa jimbo lile,, barabara za kata na mitaa ni changamoto kubwa sanaaa kwa mji wa mwanza wenye vyanzo vingi sana vya mapato ikiwemo utalii ,uvuvi,migodi,usafirishaji,ambapo NYAMAGANA ni center ya hifadhi NA KIUNGO CHA MIKOA YOTE YA KANDA YA ZIWA,, mji una hotel nyingi sana za kisasa na kitalii,rasilimali za madini Uvuvi nk....
Maji bado ni changamoto kubwa sana wakati mji wa NYAMAGAMA umezungukwa na rasilimali nyingi sana Pamoja na ziwa victoria ambacho ni chanzo kizuri cha maji....alakini bado wananchi wanapata taabu ya maji.

Ndugu zangu wana NYAMAGANA mnahitaji kijana atakayeweza kuendana na siasa za speed kubwa kwa maendeleo ya haraka sanaaa...... Kijana wenu kamanda FAIDA POTEA Mjukuu wa Njelekela niliye kuwa na PEPERUSHA BEDERA YA WA TANZANIA KWENYE MASHIRIKA Makubwa DUNIANI,, nakuja kujitosa ili jamii yangu inufaike na elimu yangu na nguvu yangu...NA KILE WAZUNGU WANACHO nufaika nacho kwangu .

Naomba mnipokee ili tupate maendeleo ya haraka sanaa,, Mimi ni mtoto wenu nimesomea shule yenu ya wazawa, sasa naomba muonje matunda ya mtoto wenu ambaye ni zao la shule zenu za uhuru, nazijua changamoto zilizopo kwenu, maisha yenu nayajua vizuri,, familia yangu ni ya kimaskini sana, naamini nitawatumikia kwa upendo na unyenyekevu wa hali ya Juu.

Ahsanteni sanaaa Mungu awe kiongozi wetu daima.... CCM ni yetu wote

Wenu,
poteafaida@yahoo.co.uk --kijana wa mwanza kutoka JUMUIYA YA WAZAZI

Ameandika hayo Faida Potea Katika Mtandao wa WhatsApp na Facebook
 
Back
Top