Je AI itauwa ubunifu, ama kudhoofisha taaluma?

Kasomi

JT Founder
Je AI itauwa ubunifu, ama kudhoofisha taaluma?
Tupo katika kipindi ambacho, tafiti nyingi zinahitajika kuhusu athari za AI kwenye ubunifu na taaluma.

Wakati calculator za kidijitali zilipoanza kutumika, baadhi ya watu walihofia kuwa hazitahitajika tena akili za wanahisabati. Wengine walihisi kuwa wataalamu wa hesabu watapoteza nafasi zao. Lakini leo tunajua kuwa calculator haikumaliza taaluma ya hesabu – badala yake, ilirahisisha kazi na kuongeza ubora wa uchambuzi wa kihisabati.

Mfano mmoja ni sekta ya uhandisi: licha ya uwepo wa kalkuleta na kompyuta, bado wahandisi hujifunza hisabati kwa kina – kwa sababu vifaa hivyo ni vya kusaidia, si vya kuchukua nafasi ya maarifa.

Sasa tupo kwenye zama za AI. Programu kama Copilot, ChatGPT, na zana nyingine zinaweza kusaidia kuandika msimbo (code). Kwa mujibu wa Microsoft, zaidi ya 30% ya msimbo wa programu unaandikwa na AI kwa sasa. Hii imesababisha baadhi ya wanafunzi na watengenezaji kuamini kuwa hawahitaji tena kujifunza lugha za programu – kwamba AI itawafanyia kila kitu.

Credit: Bongoclass
 
Back
Top