Jinsi ya kulipwa $49/task kwa kuwa na Laptop ama simu ya mkononi pekee

Kasomi

JT Founder
Jifunze namna unaweza kuingia hela mtandaoni kwa kutest website na apps mbalimbali.

Testing ni moja ya process muhimu sana kwa kampuni za Teknolojia kufanya kabla hawajapeleka bidhaa yeyote sokoni.Kampuni huwa zinatofautiana namna ambavyo huwa zinatest product zao, nyingine huwa wana timu yao ya ndani ya kutesti na wengine huwa wanatafuta random testers kutest bidhaa zao.
Kwenye makala hii nitazungumza kuhusu website ambayo inatoa kazi mbalimbali za kutest website tofauti tofauti.

Disclaimer: Kabla uendelee kusoma ningependa kukufahamisha ya kwamba makala hii ina link za referall ambapo ukijisajili kupitia link yangu na ukafanya kazi kuna kiasi kidogo nitalipwa. Unaweza ishia hapa ama kuendelea incase huna tatizo na hili.
Testa io ni nini?
Testa ni kampuni ambayo ina partnership na makampuni mbalimbali ya Teknolojia kwa ajili ya kutest product zao na kisha hulipwa na wao kulipa freelancers baada ya kazi kuisha.
Baadhi ya makampuni makubwa ambayo yanaushirikiano na Testa ni pamoja na 1X bet, Playgon na live 88.
Vitu gani huwa Testa wanatoa kazi kuvitest?
  • Onboarding test: Hapa utatest mfumo wa kujisajili wa website mbalimbali na namna zinavyofanya kazi na utatoa feedback kama zinafanya kazi vizuri ama kuna changamoto umepitia.
  • Payment Testing: Hapa utatest kama njia za malipo kwenya app mbalimbali kama unafanya kazi ama haufanyi kazi.Kazi utakazopewa hapa ni kama zile za kuwithdraw na kudeposit then utatoa feedback kama inafanya kazi vizuri ama vibaya.
  • Bonus testing:Website nyingi huwa zina sytem za kutoa bonus na reward kwa wateja wao. So hapa utapewa test kadhaa utest mifumo ya bonus kisha utoe feedback zako ya namna zinafanya kazi.
  • Perfomance testing; Hii sana sana huwa inapendwa na kampuni za gaming, ambapo watakupa game zao ujaribu kucheza na utoe feedback namna ambavyo zinafanya kazi.
  • Localization testing: Hapa utapewa utest website ama app kwenye lugha tofauti tofauti kulingana na lugha ambayo umejaza kwamba unaweza kuzungumza ama kuiandika.
  • Compatibility test: Hapa utajaribu utest kama app/website inafanya kazi kwenye aina tofauti tofauti za vifaa. so unaweza ambiwa utest website fulani inavyofanya kazi kisha utoe feedback, so kigezo pekee hapa ni ujaze list ya device zote ambazo uko nazo.
Huwa wanatoa kazi mara kwa mara?
Mara zote nimependa kuwa mkweli, Testa.io huwa hawanitumii kazi mara kwa mara ila wakinitumia huwa zinakuja na maziwa(hela) fiti. Frequency ya kupata kazi Testa huwa inategemeana na namna umefanya kazi ya kwanza, location pamoja na no ya vifaa uko navyo.

Screenshot_2025-12-31_at_11.51.44.png

Kazi ya $49 ambayo ninaifanya sasaivi
Huwa wanalipa kwa njia ipi?
Testa wanalipa kwa njia ya Wise. Changamoto kubwa ambayo iko Wise now ni hawatoi akaunti za USD kwa watanzania ila sisi wakongwe wa zamani tuko nazo.Ushauri wangu wewe piga kazi hela ikiwepo kutoa hutoteseka.
Namna ya kujisajili Testa
Ingia kwenye website ya Testa kisha sign up ukisubiri kupewa kazi.
 
Back
Top