Daktari wa upasuaje afungwa miaka 20 kwa kubaka watoto

Kasomi

JT Founder
1748442707701.jpg

Joel Le Scouarnec, daktari wa zamani wa upasuaji nchini Ufaransa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela siku ya Jumatano baada ya kukiri kuwanyanyasa wagonjwa 299 wengi wao wakiwa watoto.

Daktari huyo mstaafu alikiri kuwafanyia vibaya jumla ya wagonjwa wa kiume 158 na wanawake 141 wa wastani wa umri wa miaka 11 kati ya 1989 na 2014.

Waendesha mashtaka walimshutumu kwa kuwatendea wagonjwa wake kama "vitu visivyo na uhai", kutoonyesha huruma yoyote, na kutumia vibaya nafasi yake kama daktari.

Wamesema mara nyingi aliwanyanyasa wagonjwa ambao bado walikuwa wamelala baada ya kuchomwa dawa ya usingizi ama nusu kaputi au watoto ambao hawakuweza kuainisha matendo yake kama unyanyasaji.

Kesi hiyo imeibua maswali juu ya sababu hasa za mamlaka kushindwa kumzuia daktari huyo mapema kwa kuwa tayari alihukumiwa kifungo cha nje kwa kuyanyasa kingono watoto mwaka 2005.
 
Back
Top