Kasomi
JT Founder
MICHEZO: Mshambuliaji mpya wa Al Ahly ya Misri, Mahmoud Hassan maarufu kama Trezeguet, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kukosa mkwaju wa penalti katika mchezo wao dhidi ya Inter Miami katika michuano ya Kombe la Dunia la Kilabu.
Katika mchezo huo uliochezwa Jumapili usiku kwenye Uwanja wa Hard Rock, Marekani, mabingwa hao wa Misri walitoka suluhu na Inter Miami ya Marekani anayochezea Lionel Messi.
Tukio lililozua gumzo kubwa lilitokea dakika tano kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika, ambapo Al Ahly walipata penalti baada ya Zizo kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Hata hivyo, sintofahamu ilizuka baada ya Trezeguet kuchukua jukumu la kupiga penalti hiyo, licha ya kuwepo kwa mpangilio wa timu unaomtaja mshambuliaji, Wissam Abu Ali kama mpigaji wa kwanza wa penalti.
Hivyo Al Ahly wameamua kumtoza faini Trezeguet kufuatia kitendo chake wakati wa mkwaju wa penati dhidi ya Inter Miami kwenye Kombe la Dunia la Klabu.
Je, Uamuzi huo wa haki au mkali sana
Chanzo: EastAfricaTV