Advertise here

Faustine Mafwele apigwa marufuku kuingia Marekani

Kasomi

JT Founder
1000697532.jpg

Marekani imetangaza kumwekea vikwazo afisa mwandamizi wa polisi ya Tanzania Faustine Jackson Mafwele kwa tuhuma za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na ukandamizaji wa raia.

Tangazo la uamuzi huo limetolewa na Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani na kuchapishwa rasmi kwenye tovuti ya wizara hiyo usiku wa kuamkia leo. Washington imesema inazo taarifa za uhakika za kuhusika kwa Mafwele na vitendo vya ukandamizaji haki za binadamu na ukatili.

Mojawapo ni kisa kilichotokea mwaka jana cha kukamatwa, kuteswa na kufanyiwa vitendo vya kutweza utu wanaharakati Agather Atuhaire kutoka Uganda naBoniface Mwangi wa Kenya waliokwenda Tanzania kufuatilia kesi iliyomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. Chini ya hatua hizo za vikwazo Mafwele hatoruhusiwa kuingia nchini Marekani.
 
Back
Top