Advertise here

Wachokonozi wadaiwa kukamatwa

Kasomi

JT Founder
1750453997222.jpg

Vijana wawili Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo wanaounda kundi la "Wachokonozi" wamevamiwa na watu wenye silaha waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi wakiwa nyumbani kwao maeneo ya Maji ya Chai, wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao walikuja na gari aina ya Landcruzer wakiwa wamevalia kiraia na wamebeba silaha za moto. Walipoingia ndani waliwaweka vijana hao chini ya ulinzi lakini walipoambiwa watoe vitambulisho kuthibitisha kama wao ni Polisi kweli walikataa.

Walifanya upekuzi kwenye nyumba hiyo bila kufuata taratibu. Walipoambiwa waitiwe mjumbe wa serikali ya mtaa ili awe shahidi walikataa, na kusema wasifundishwe kazi. Katika upekuzi huo wamechukua vifaa mbalimbali ikiwemo camera, computer, microphones, tape revorder, na nyaraka mbalimbali zilizokuwemo, kisha kuwafunga pingu "Wachokonozi" na kuondoka nao.

Majirani walipouliza wanawapeleka kituo gani cha Polisi, watu hao hawakujibu bali waliondoa gari kwa mwendo mkali. Ndugu wameenda kituo cha Polisi Maji ya Chai lakini hawajawakuta. Hadi sasa, haijafahamika wamepelekwa kituo gani lakini ndugu wanaendelea kufuatilia.

Familia za "Wachokonozi" zinaomba tuwasaidie kupaza sauti ili ndugu zao wapatikane wakiwa hai. Wanaomba waliowakamata wasiwaue wala kuwapoteza bali kama wanatuhumiwa kwa makosa yoyote basi wawapeleke mahakamani kwa hatua za sheria.!
 
Back
Top