Kasomi
JT Founder
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kulwa Biteko, amefika katika Ofisi za CCM wilaya ya Geita majira ya saa 2:30 asubuhi hii kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Katoro, linalopatikana katika Mamlaka ya Mji Mdogo Katoro, Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Kulwa amepokelewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Geita, Michael Msuya.
Hii ni mara ya pili kwa Kulwa Biteko kuchukua fomu ya ubunge, ambapo mwaka 2020 alishinda kura za maoni katika Jimbo la Busanda lakini hakuteuliwa kuwa mgombea. Kwa sasa, jimbo hilo limegawanywa kuwa majimbo mawili: Jimbo la Katoro na Jimbo la Busanda.
Kulwa Biteko ni pacha wa Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.