Maelekezo Ya Kujiunga Na Shule Ya Sekondari Bugando Halmashauri Ya Wilaya Ya Geita Kidato Cha Tano Mwaka 2024/2025

Kasomi

JT Founder
MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI BUGANDO
HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA KIDATO CHA TANO MWAKA 2024/2025.

2. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:
1. SARE ZA SHULE.
(a) Sare ya shule hii ni mashati mawili (2) meupe ya tetron yenye mikono mirefu.
(b) Suruali mbili(2) rangi ya kijivu giza zenye malinda manne (4) (malinda mawili upande wa kulia
na mawili upande wa kushoto.
(c) Sare ya michezo ni trucksuit na kaptula mbili (02) za rangi ya bluu ivuke magoti siyo suruali
ikiwa na vest yake vinauzwa pamoja.Hakikisha unakujanavyo, Kumbuka pia kuja na raba jozi
moja (1) kwa ajili ya michezo.
(d) Viatu vya shule ni vyeusi vya ngozi vya kufunga na kamba vyenye visigino vifupi jozi mbili.
(e) Soksi fupi jozi mbili (2) rangi nyeusi.
(f) Mkanda wa kuvalia suruali ni mweusi wa ngozi.
(g) Sweta rangi ya dark bluu inapatikana madukani.
(h) -Nguo za kushindia ni tisheti ya shule rangi ya dark blue yenye kola ya rangi ya kakiSuruali ya kushindia rangi nyeusi yenye malinda mawili kila upande.
KUMBUKA:Shati la shule litachomekewa muda wote unapovaa sare ya shule.

2. UVAAJI WA SARE YA SHULE.
Sare ya shule inavaliwa wakati wote wa masomo,baraza,mihadhara na wakati Mwanafunzi
anapokwenda nje ya mipaka ya shule kama vile kanisani, msikitini n.k.T.shirt ya shule ivaliwe shuleni
tu wakati usio wa masomo na sweta livaliwe wakati wa Baridi tu. Majaketi,kofia,makoti,na mapambo
mengine haviruhuisiwi kuvaliwa kabisa pamoja na sare ya shule.Hivyo atakayeonekana na mavazi
tofauti na yaliyoainishwa Hapo juu atachukuliwa hatua za kinidhamu.

KUMBUKA: NGUO ZINGINE ZOZOTE TOFAUTI NA SARE YA SHULE HAZIRUHUSIWI
KUVALIWA SHULENI NA NJE YA SHULE NA IKITOKEA UMEZIVAA ZITAKAMATWA NA
HAZITARUDISHWA NA HATUA KALI ZA KINIDHAMU ZITACHUKULIWA DHIDI YAKO

3. MICHANGO YA SHULE.
Mwanafunzi wa bweni atalipa Michango kwenye akaunti ya shule,
SHULE YA SEKONDARI BUGANDO AKAUNTI NAMBA 31001100550 KATIKA BENKI YA NMB.
Unatakiwa ukabidhi stakabadhi kabla Hujasajiliwa (tafadhali andika jina la mwanafunzi, kidato na
tahasusi yake nyuma ya stakabadhi au pay in slip).

. MICHANGO YA SHULE.
Mwanafunzi wa bweni atalipa Michango kwenye akaunti ya shule,
SHULE YA SEKONDARI BUGANDO AKAUNTI NAMBA 31001100550 KATIKA BENKI YA NMB.
Unatakiwa ukabidhi stakabadhi kabla Hujasajiliwa (tafadhali andika jina la mwanafunzi, kidato na
tahasusi yake nyuma ya stakabadhi au pay in slip).
(a) KWA WANAFUNZI WA BWENI
Na Aina ya Mchango Kiasi
1 Mchango wa Uendeshaji wa Shule 65,000/=
2 Tahadhari 5,000/=
3 Nembo 5,000/=
4 Kitambulisho cha shule 5,000/=
Jumla 80,000/=
➢ MUHIMU: Mwanafunzi aje na Bima ya Afya au kama hana aje na Pesa kwa ajili ya
bima Tshs. 50,400/= (Fedha taslimu).

4. MAHITAJI MUHIMU AMBAYO MWANAFUNZI ANAPASWA KULETA SHULENI NI:
(a) Ream mbili za karatasi (2) aina ya A4 (kwa mwaka).
(b) Vitabu vya masomo ya tahasusi husika.
(c) Scientific calculator silent non programmable with function ranging from FX-82 to Fx-991 kwa
wale wanaosoma tahasusi za HGL, PCB na PCM na mathematical set.
(d) Dissecting kit kwa wale wanaosoma tahasusi ya PCB
(e) Godoro kwa wanafunzi wa bweni futi 6 kwa futi 2.5
(f) Shuka jozi mbili (rangi ya pink), blanketi-1,foronya-1,chandarua-1(shuka la kimasai
hairuhusiwi na halitambuliki kama shuka au blanketi)
(g) Vyombo vya chakula (sahani,bakuli,kijiko na kikombe)
(h) Ndoo mbili ndogo zenye mifuniko.
(i) Jembe na mpini (kwa wanafunzi wa PCB na PCM tu)
(j) Kwanja-1,reki-1, mfagio wa ndani (soft bloom)-1 na Mfagio wa nje (chelewa)-1 na mopper-1.
(k) Shoka na mpini (kwa wanafunzi wa HGL tu).
(l) Jalada (file cover) la kutunzia kumbukumbu zako.
(m)Vifaa vya usafi (mswaki, dawa ya meno,dawa ya viatu, kioo,Kitana ,kanda mbili, taulo nk)
(n) Madaftari (counter books) yasiyo pungua saba (7), madaftari ya kawaida na Grafu kwa ajili
ya mazoezi.
(o) Sanduku imara na kufuli madhubuti kwa ajili ya kutunzia mali zako.
(p) Dumu la lita 5 la kutunzia maji ya kunywa.
5. MAKOSA YATAKAYO SABABISHA MWANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE:
(i)Wizi.
(ii)Kutohudhuria masomo kwa Zaidi ya siku tisini bila taarifa/utoro.
(iii)Kugoma au kuhamasisha mgomo.
(iv)Kutoa lugha chafu kwa wanafunzi wenzake, walimu,walezi na jamii kwa ujumla.
(v)Kupigana mwanafunzi kwa mwanafunzi, kumpiga mwalimu au mtu yoyote yule.
(vi)Kufuga ndevu au kufuga nywele.
(vii)Wanafunzi wote wanatakiwa kuwa na nywele fupi wakati wote wawapo shuleni.
(viii)Ulevi au unywaji wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya.
(ix)Uvutaji wa sigara.
(x)Uasherati, mahusiano yajinsia moja au kuoa.
(xi)Kushiriki matendo ya uhalifu, siasa na matendo yoyote yale yanayovunja sheria za nchi.
(xii)Kusababisha mimba au kumpa mimba msichana.
(xiii)Kutembelea majumba ya starehe na nyumba za kulala wageni.
(xiv)Kumiliki, kukutwa au kutumia simu ya mkononi katika mazingira ya shule.
(xv)Kudharau bendera ya Taifa.
(xvi)Kufanya jaribio lolote la kujiua au kutishia kujiua kama kunywa sumu nk.
(xvii)Uharibifu wamali za umma kwa makusudi.

6. VIAMBATANISHO NA FOMU MUHIMU.
• Fomu ya uchunguzi wa afya (medical examination form) ambayo itajazwa na mganga mkuu
wa hospitali ya serikali.
• Fomu ya maelezo binafsi kuhusu historia ya mwanafunzi/mkataba wa kutoshiriki Katika
mgomo,fujo na makosa yajinai.
• Fomu ya mzazi kukiri kukubaliana na sheria, kanuni, kulipa michango na maelezo mengine
yatakayotolewa na shule.
• Picha nne (4) za wazazi na ndugu wa karibu na mwanafunzi wanaoweza kumtembelea
mwanafunzi shuleni pamoja na namba zao za simu.
• Sheria na kanuni za shule ya sekondari ya Bugando.
• Kivuli cha matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2022
• Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
7. Tafadhari soma kwa makini maelezo/maagizo haya na kuyatekeleza kikamilifu.

KIAMBATANISHO A
A. ORODHA YA VITABU KWA KILA TAHASUSI (COMBINATION)
GENERAL STUDIES REFERENCE BOOKS
1. Richard R.F Mbalase (2011), General Studies for forms 5 & 6
2. General studies For Advanced level Certificate; Afroplus Industries Ltd.
3. James Bigiramungu & Deogratias S.M (2012), Understanding Advanced level General Studies
PHYSICS REFERENCE BOOKS
1. Mehta.v.k, (2013) S. Chand’s principles of Physics for Class xll 7th ED,S. Chand & Company
pvt Ltd, New

CHEMISTRY REFERENCE BOOKS
1. Jain.S.K,(2010),Conceptual chemistry For Classx1,S.Chand & Company Ltd New Delhi, india.
2. Bahl. B.S et al (2009), Essentials of physical chemistry, s, chand & company Ltd, New Delhi,
india.
3. Ramsden. E.N, (2000), A-Level chemistry, 4th Ed, Nelson Thorns Ltd, U.K.

BIOLOGY REFERENCE BOOKS.
1. Taylor D.J,(1999),Biological Science,3rd Ed,Cambridge University Press London.
2. Understanding Biology

ADVANCED MATHEMATICS REFERENCE BOOKS.
1. Horril.P.J.F.(1985),Pure Mathematics Book 2,3rd Ed, Longman Group Limited, London.
2. Tranter. C.J. (1975), Advanced level pure mathematics, 4th Ed, Hodder & Stoughton,
London.
3. Dass. H. K & Verma, R. (1997) S.chand’smathematics for class xii (volume ii), S.chand &
Compan ltd. New delhi.

ENGLISH LANGUAGE REFERENCE BOOKS
1. Francis Mnyawi, Contemporary English.
2. Nicolous Ashel (2016), Advanced English Language
3. Ndambo, English Language for Advanced Level; Nyambari Nyangwine.

GEOGRAPHY REFERENCE BOOKS
1. Bunnett R.B (2006), General Geography in Diagrams, Pearson Education South Asia, Ptc Ltd
Singapore.
2. Monk House F.J(1975), Principles of Physical Geography.
3. Leong C.G and Morgan C.G (2009), Human and Economic Geography, Oxford University
Press. UK
4. Avelius Thobias (2001), Fundamental in Advanced Level Practical Geography, Mwagomba
Press, Dar es Salaam. (kinapatikana shuleni kwa Tshs.16,000/=)

HISTORY REFERENCE BOOKS
1. Avelius Thobias (2001), Fundamental in Advanced Level History 1, Mwagomba Press, Dar es
Salaam. (kinapatikana shuleni kwa Tshs.16,000/=)
2. Avelius Thobias (2001), Fundamental in Advanced Level History 2, Mwagomba Press, Dar es
Salaam. (kinapatikana shuleni kwa Tshs.16,000/=)

Bonyeza Hapa kudownload Fomu
Download Bugando Secondary School (S1127) Joining instruction form five
 

Similar threads

Back
Top