Captain Tesha ajitoa muhanga kuongea hatari ya Taifa linapoelekea

Mtata

Member

Kupitia YouTube, Kapteni Tesha anaanza kwa kusema..

"Habari za wakati huu watanzania Kwa majina naitwa Captain Tesha afisa kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania katika kikosi [00:03] cha Saki kwa maana kwamba ni shule ya anga ya kijeshi Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu [00:13] na nchi kwa kunipa uhai na afya mpaka muda huu ambapo nazungumza nanyi Watanzania wenzangu nikiwa na maumivu makubwa sana [00:21] moyoni juu ya haya yanaendelea katika nchi yetu...""

Muhtasari.
Kapteni K. Tesha, afisa anayejitambulisha kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Saki/Shule ya Anga ya Kijeshi), anatoa maoni yake kwa umma kuhusu hali anayoiona katika taifa.

Hoja Kuu za Kapteni Tesha:
Hatari ya Taifa: Anadai anaona hatari kubwa mbele ya taifa kutokana na yale yanayoendelea [00:30]. Anasema ametoa barua kwa wakubwa wake, akiwemo CDF, kuonyesha kutoridhishwa kwake na hali ya nchi [01:35].

Jeshi Kuchukua Nchi: Anashauri Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ) lichukue nchi haraka ili kuweka mambo sawa, akidai kuwa imani pekee ya Watanzania imebaki kwenye jeshi [02:34]. Anataka uchaguzi uzuiwe kwa sababu una mtego na umejaa makashfa [01:00:25].

Deep State: Anaelezea dhana ya "Deep State" kama kundi la watu wenye ushawishi ndani ya serikali au taasisi za dola (serikali ndani ya serikali) ambalo linaendesha maamuzi nyuma ya pazia [04:19]. Anadai kundi hili nchini linaongozwa na "CCM Mtandao" wakiwemo Mstaafu Kikwete na Rostam Aziz.

Uchunguzi wa Kifo cha Magufuli: Anasisitiza kuwa kifo cha Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli kichunguzwe na Jeshi kwa haraka, akitaja taarifa kwamba kinaweza kuwa kimesababishwa na CCM Mtandao.

Ushauri kwa CDF: Anamuomba CDF (Mkuu wa Majeshi) asikubali siasa kuingizwa Jeshini kwa kuwa inaweza kugawanya umoja wa jeshi, na anashauri Kikwete na mtandao wake wakamatwe kujibu tuhuma za ufisadi na kifo cha Magufuli.
maxresdefault (1).jpg
 
Wanasema eti sio kweli ni akili mnemba imetumika!na imekanushwa!!Kuna comrade kaniambia hilo!!

Ngoja tuone uvumi huu utakua na impact gani kuelekea uchaguzi!
Kwa Madai ya AI hiyo hapana ile ni human kabsa sio ai labda wasema yule sio Mwanajeshi basiii ila kusema ni teknolojia picha za kutengenezwa zinajulikana tena na alivyo ongea kwa muda mrefu vile
 
Wanasema eti sio kweli ni akili mnemba imetumika!na imekanushwa!!Kuna comrade kaniambia hilo!!

Ngoja tuone uvumi huu utakua na impact gani kuelekea uchaguzi!
Ile Sio AI
Fact hizi hapa
 
Ile Sio AI
Fact hizi hapa
Kwahiyo ni rasmi kimenuka!!?tutarajie fireworks.kati ya jwtz mtandao dhidi ya jwtz wazalendo!!?
 
Back
Top