Je, JWTZ imejibu Hoja Ya Captain Tesha?

Mtata

Member
JE, JWTZ IMEJIBU HOJA YA CAPT. TESHA?

Anaandika Emmanus Bandekile Mwamakula

Baada ya Capt Tesha kutoa hotuba kwa njia ya video, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa kauli kwa njia ya waraka. Hata hivyo, waraka huo unafichua ya kuwa baadhi ya hoja hizo hutolewa na:

1. Watu walio katika mazingira ya kijeshi.

2. Watu wanaojinasibisha na Jeshi.

3. Watu walioachishwa Jeshi kwa tabia mbaya

4. Watu walioachishwa Jeshi kwa kujihusisha na siasa na wanaharakati.

Waraka huo haujakanusha ukweli wa maudhui yaliyomo katika hotuba ya Capt. Tesha. Lakini pia, waraka huo umekwepa kumzungumzia mtu aliyejitambulisha kama Capt. Tesha, hivyo Jeshi halijasema kama Capt. Tesha ni askari aliye kazini au la, na pia kama ni askari au mtu anayeangukia katika aina kundi lipi kati ya hayo manne hapo juu, Jeshi halijasema.

Kwa ujumla, kauli ya Jeshi haijajibu maswali bali imezidi kuongeza maswali na hivyo kuzidi kuwafanya watu wazidi kusikiliza hotuba ya Capt. Tesha kuliko kuipuuza. Ni wazi kabisa ya kuwa Capt. Tesha ni phenomona iliyoibuka kwa ghafla bila ya kutegemewa. Kwa sababu hiyo, ili kuikabili phenomona kama hiyo huhita tafakuri nzito na hekima ya hali ya juu.

Ukurasa wa askofu unawaalika watu kujadili na kutafakari juu ya ukweli au uwongo ulio katika hoja za Capt. Tesha badala ya kujadili, kutaka kujua kikosi chake au hata hali yake ya ajira ya jeshini kama ni hai au mfu. Tukiazima kauli ya Kikwete, "hoja haipigwi rungu'! Kwa hiyo tujadili au kujibu au tukanushe hoja ya Capt. Tesha.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 4 Oktoba 2025; Saa 4:00 usiku
 
Back
Top