Kasomi
JT Founder
Kurasa rasmi za Instagram na Facebook za aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Zimefungwa. Hapo awali baada ya account hizo kutokuwepo hewani zilizua taharuki kubwa kwa watu waliokuwa wakimfatilia baada ya kuripotiwa kutekwa kwake siku ya jana Oktoba 6, 2025
Baadae leo mwanaharakati Maria Sarungi Tsehai ametoa taarifa kuwa alitoa ripoti kwenye kampuni husika ya meta wamiliki wa facebook na instagram ili kuweka usalama wa akaunti hizo.
"Tuneweka akaunti za Humphrey Polepole salama ili wahuni wasiweze kuzifikia, hakuna aliyezifuta zimehifadhiwa until Polepole atakaporudi uraiani.
Tunashukuru kampuni za mitandao zime react fasta! Mwambieni Mafwele sasa wamwachie hawapati kitu hapo!" Ameandika Maria Sarungi.