Øffïçïäl Dülly Tz
New member
Story.........PENZI LA MTEKAJI
Present.....Simulizi Za Dully
Mtunzi.....Official Dully Tz
WhatsApp...0628924768
Mkasa..wa..kusisimua
Sehemu..Ya..{01}
(Seaeon two)
Yapata majira ya saa saba usiku, kiza kinene kilikuwa kimeshamiri kila pande ya jiji la Dar es salaam pia jiji lilikuwa limetulia na kila mkazi wa jiji hilo alikuwa amejipumzisha ndani ya nyumba yake au sehemu ambayo hupumzika ifikapo majira ya usiku.
Wakati jiji limetulia ghafla ilionekana gari moja nyeusi ikikimbia kwa kasi sana na mwisho gari hiyo ilifika sehemu iliyokuwa na kiza kinene na kusimama kisha ilizimwa.
Baada ya gari hiyo kuzimwa hazikupita hata dakika tatu yalionekana magari ya polisi yapatayo manne yakipita kwa kasi na hii iliashiria gari hiyo ilikuwa ikikimbizwa na polisi.
Polisi walikuwa hawajaiona gari hiyo maana ilikuwa kwenye kiza kinene hivyo baada ya kupita ile gari ilitoka taratibu na kutokomea pasipo julikana na haikufahamika kwanini ilikuwa ikikimbizwa na polisi.
Basi tutoke huko sasa tuje upande wa pili nyumbani kwa tajiri mmoja mkubwa ndani ya jiji la Dar es salaam ambae usiku huo alikuwa na huzuni sana sambamba na mke wake pia polisi nao walikuwa wamekusanyika wengi kwenye nyumba hiyo kuashiria kuna tatizo limetokea.
"Pole sana Mr Mbega tunajua kiasi gani upo na majonzi sana kwa kutekwa binti yako lakini usijali naamini atapatikana ila tungependa kufahamu ametekwaje au alikuwa safarini.!?"
Lilikuwa ni swali kutoka kwa askari mkubwa wa polisi ambae alifika hapo kwaajili ya kumuhoji Mr Mbega aliekuwa na huzuni sana usiku huo.
"Afande unajua binti yangu ni mtu anaependa sana starehe sasa usiku wa leo alikuwa ametoka na rafiki zake na aliniaga amesema sijui kuna birthday sasa wakati anarudi ndio ametekwa kwa mujibu wa taarifa tulizopewa na rafiki zake"
"Ahaa kwahiyo hujapata kujua ni kina nani wamemteka nikiwa na maana huenda ni wapinzani wako wa kibiashara au vibaka tu wanataka pesa kutoka kwako.!?"
"Afande mimi sifahamu kabisa yaani daah nilipigiwa tu simu na binti yangu nilipopokea nilimsikia akipiga kelele kuomba msaada na muda huo huo ukimya ukatawala sikumsikia tena"
Mr Mbega alijieleza vizuri na polisi walikuwa wakichukua maelezo yake ili kuanza uchunguzi na kujua binti yake atakuwa wapi na kumpatia msaada.
Polisi baada ya kuchukua maelezo kwa Mr Mbega walimuaga na kuondoka zao huku nyuma wakimuacha akiwa na majonzi pamoja na mke wake ambae alikuwa akilia muda wote kama mtu aliefiwa.
"Mke wangu hebu nyamaza basi mimi naamini lazima binti yetu Karina atakuwa sawa na tutampataa maana jambo likifika mikononi mwa polisi kila kitu kitakuwa sawa ondoa shaka"
"Ni sawa mume wangu lakini yote haya wewe ndio sababu yaani mimi nilitaka hata asiende huko lakini wewe kwa kumpenda sana umemruhusu na matokeo yake ni haya sasa"
Mke wa Mr Mbega alikuwa mwenye majonzi na lawama zote alizimwaga kwa mume wake lakini wakati huo huo alitoka kijana wake mkubwa ndani akiwa na simu ambayo ilikuwa ikiita.
Alifika mpaka alipo baba yake na kumpatia maana simu hiyo ilikuwa ni simu ya baba yake lakini namba iliyokuwa ikipiga ilikuwa ni namba ngeni hivyo Mr Mbega baada ya kupokea alisikia binti yake akipiga kelele upande wa pili na muda si punde sauti nzito ya kiume ilisikika.
"Najua unaumia sana kusikia sauti ya mtoto wako Mr Mbega lakini tuache hayo ninachotaka ni kitu kimoja tu, pesa yaani kama ukileta pesa basi binti yako tutamuacha kwahiyo tutakupa siku mbili tu tunahitaji milion hamsini, sasa ni muda wako wa kuchagua umuache binti yako ateseke au ulete pesa kumkomboa"
Mwanaume huyo baada ya kuzungumza hakutaka kumpa mafasi ya kuzungumza Mr Mbega, alikata simu na kumfanya Mr Mbega achanganyukiwe asijue afanye nini ili kumkomboa binti yake Karina.
"Mume wangu vipi tena mbona umepoa ghafla baada ya kupokea hiyo simu, kuna habari gani mbaya imetokea.!?"
Mke wa Mr Mbega alijikuta akiuliza kwa hofu huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana lakini Mr Mbega hakutaka kumjibu zaidi ya kumtaka kijana wake wapande gari na kuelekea bank kutoa pesa.
"Baba tunaenda wapi na ile simu ilikuwa imahusu nini au mdogo wangu Karina atakuwa tayari ameuwawa maana nashindwa kuelewa kabisa.!?"
Wakiwa kwenye gari mtoto mkubwa wa Mr Mbega ambae alifahamika kwa jina la Godwin alimuuliza baba yake ambae alikuwa makini kwenye usukani.
"Wanataka pesa"
"Wanataka pesa, wakina nani hao wanataka pesa.!?"
"Hao watu waliomteka Karina wanataka pesa ili kumuachia kwahiyo tunaelekea bank kuchukua pesa pia ikiwezekana tuwataarifu na polisi ili iwe salama na sisi kwa upande wetu!"
Mr Mbega alizungumza huku akiwa makini barabarani lakini muda huo huo simu yake iliingia message, alipoitazama ilikuwa ni location ambayo alitakiwa kufika na pesa pia ilimuonya asithubutu kwenda na polisi vinginevyo atamkosa binti yake.
"Shiit wamesema tusiende na polisi la sivyo atamuuwa Karina sasa hapa ni kutumia akili tu vinginevyo tutatoa pesa alafu binti yangu nisimpate"
"Lakini hata mimi nilikuwa naona tutii kauli yao tusiende na polisi kwasababu nakumbuka kipindi nipo uturuki lilitokea tukio kama hili mwanafunzi mwenzetu alitekwa na baba yake aliambiwa atoe pesa ila asiende na polisi lakini alikaidi mwisho kijana wake aliuwawa kwahiyo twende tu naamini tutampata Karina"
Mazungumzo na ushauri ulikuwa ukiendelea kati ya baba na mtoto huku safari ikizidi kusonga na mwisho walifika katika bank na kushuka ili kwenda kutoa pesa ya kumkomboa Karina kutoka kwenye mikono ya watekaji.
**************
Huku upande wa pili kwa watekaji walikuwa kwenye jumba moja kuu kuu ambalo ndipo waliweka makazi yao na jumba hilo lilikuwa kando kidogo ya maji.
Walikuwa watekaji wanne wote walivalia nguo nyeusi juu mpaka chini lakini Miongoni mwa watekaji hao alikuwa kijana mmoja wa makamo kwa kumtazama alikuwa na miaka 23 nae pia alikuwa ni mtekaji.
Kijana huyo licha ya kuwa mtekaji lakini pia alikuwa ni mwanafunzi wa chuo na alifahamika kwa jina la Brey, kijana ambae alikuwa akiishi maisha magumu ila wazazi wake wote wawili walikuwa kijijini.
Karina alikuwa ameketi chini mikononi akiwa amefungwa kamba pia mdomoni alikuwa amezibwa ili asipige kelele ambazo zingeweza kuwagharimu na kuwafelisha mpango wa kupata pesa.
"Sasa sikieni niwaambie jamani, mimi nikiwa kama ndiye kiongozi wa kundi hili, pesa kama italetwa basi Brey hutaweza kupata mgao maana wewe ndiye sababu ya sisi kukimbizwa na polisi"
"Mh hapana sio kweli Bro mimi mbona sikufanya chochote au ndio mnaanza kuleta zenu za kuleta ili kuninyima pesa.!?"
"Sisi hatujui hilo lakini pesa hupati labda usubiri mission nyingine itokee na kama inawezekana uondoke sasahivi vinginevyo tutakushoot risasi"
Mambo yalikuwa tayari yamebadilika, watekaji hao walikuwa wameanza kugeukana kabla ya pesa kupatikana na hii ilimfanya Brey kuchukia na kuamua kuja juu, hakukubali kabisa kuzulumiwa akiwa anajiona.
"Lakini broo sasa naona tunaenda mbali sana yaani kazi tufanye wote alafu pesa nisipate mh hapana kama kuuwana tuuwane tu lakini lazima pesa nipate hata damu ikimwagika.!!"
"Oh dogo una maneno ya kishujaa sana.!?"
Mmoja kati ya hao watekaji alimfuata Brey na kumkunja huku akimshushia matusi mazito ambayo yalimfanya Brey achukie sana.
"Sio kwamba najifanya shujaa broo lakini mnachotaka kufanya sio haki alafu kumbukeni huu mchongo nimewapa mim kwahiyo kama nimewapa mimi haiwezekani nisipate hata mia"
"Sasa kwani wewe unatakaje.!?"
Yule mtekaji mmoja ambae alikuwa ambele ya Brey alimpiga Brey ngumi matata iliyomfanya kuchanika sehemu kubwa ya mdomo wake na damu kumtoka kwa wingi sana.
Kilikuwa ni kitendo ambacho Brey hakukipenda hivyo ilibidi aje juu na kujikuta wakipanga mkono na wanaume hao watatu huku akiwa mwenyewe yaani ilikuwa watu watatu kwa mmoja na Brey sio kwamba alikuwa ni lele mama ila alikuwa mtu anaejiweza kwenye sector ya mapigano.
Wakati tukio hilo linaendelea Karina alikuwa kimya akiwatazama na kwenye nafsi yake alifurahi sana maana aliona kama wao watapigana na kuuwana basi itakuwa rahisi yeye kuondoka.
Marumbano baina ya watekaji hao yalianza lakini Brey kwa uwezo mkubwa aliokubwa alitumia dakika tano kuwaangusha wanaume hao japo na yeye alijeruhiwa lakini alikuwa amemaliza shughuli na kuwaacha wakigugumia kwa maumivu.
"Sasa binti hapa sio sehemu ya kukaa tena ninachoomba unifuate la sivyo ukileta ubishi nitakuuwa hapa hapa baba yako aje akute maiti yako"
Brey alizungumza huku akimfungulia Karina kamba za miguuni na kumtolea kizuizi cha mdomoni ambacho kilimfanya Karina ashindwe kuongea.
"Sasa hapa tunaondoka kimya kimya ole wako upige kelele yaani kama utapiga kelele basi nakumwaga ubongo kwahiyo kuwa mpole sawa binti.?"
"Sa...sa..sawa lakini mlimpigia baba yangu simu aje hapa sasa kama akija alafu asiponikuta unafikiri itakuwaje"
"Hebu kaa kimya na unifuate"
Brey alizungumza huku akitoka nnje kwa kuchechemea maana alikuwa ameumiza kwenye purukushani huku nyuma alifuatiwa na Karina ambae alionekana kuwa na hofu sana.
"Sasa tunakwenda wapi kakaangu jamani.!?"
"Alafu wewe binti hebu kwanza kaa kimya sitaki uongee kitu la sivyo mdomo wako utakuponza na hii ndio mara ya mwisho nakupa onyo ila kinyume na hapo basi nitakupiga risasi mimi sijali kama wewe ni pesa au laa"
Brey alizungumza akiwa anamaanisha na wakati huo walikuwa tayari wamefika nnje kwenye gari ambalo walilitumia kuja nalo hapo.
Brey alimtaka Karina apande na baada ya kupanda alimfunga macho na mdomo kisha nae aliingia kwenye gari na safari ilianza kutoka hapo huku Karina akiwa haelewi anapelekwa wapi.
**************
Taratibu za kutoa pesa zilifanyika na baada ya kumaliza Mr Mbega alijipakia kwenye gari yake akiwa na kijana wake Godwin na safari ilianza kuelekea huko ambapo aliambiwa afike.
Wakati wakiwa njiani simu ya Mr Mbaga ilianza kuita na aliekuwa anapiga alikuwa mke wake hivyo alichofanya ni kupuuzia maana alijua lazima mke wake atamuuliza kuhusu Karina ilhali bado kabisa hawakumpata.
Wakati simu aliyokuwa anapigiwa mke wake inakata basi muda huo huo namba ya wale watekaji ilikuwa inapiga hivyo haraka alipokea na kusikiliza kulikuwa na mpya gani anataka kuambiwa.
"Hello.!?"
"Hello..Hello ndio tupo njiani tunakuja ila naombeni nisikie hata sauti ya binti yangu tafadhali mimi pesa niko nazo nakuja nazo"
"Tafadhali mzee wewe njoo na pesa lakini kuhusu kumsikia binti yako haiwezekani kwasababu ni kupotezeana muda kwahiyo kuwa mpolee tafadhali"
Upande wa pili sauti ilisikika iliyojaa maumivu.
"Basi sawa tunafika hapo sasahivi"
Mr Mbega alizidi kukanyaga mafuta ili kuwahi eneo la tukio na kumkomboa binti yake lakini hakufahamu kama binti yake tayari alikuwa amechukuliwa na kupelekwa pasipo julikana.
Basi muda ulisogea na mpaka inatimu majira ya saa nane usiku gari iliyokuwa ikiendeshwa na Brey ilifika katika mtaa mmoja wa uswahilini na kusimamisha kisha alifungua mrango wa nyumba ambapo alikuwa Karina na kumtaka ashuke pia alimtoa kile kizuizi cha mdomoni ili aweze kuongea.
"Huku ni wapi, unanipeleka wapi jamani".!?
Karina alizungumza akiwa mwenye hofu sana lakini Brey alimtoa kile kitambaa machoni na kumfanya Karina ashangae mazingira waliyokuwepo.
"Hapa ni wapi.!?"
"Hutakiwi kujua kwa sasa wewe nifuate alafu nilikwambia sitaki maswali ila kama utaendelea basi nitafumua hicho kichwa chako"
Brey alitoa maneno ya vitisho na kumfanya Karina awe mpole lakini mpaka wakati huo Karina hakuona sura ya Brey maana alikuwa na mask usoni mwake.
Walitembea kwa takribani nusu saa hatimae walifika katika nyumba moja iliyokuwa na kiza kinene, haikujulikana ilikuwa ni nyumba ya nani lakini Brey baada ya kufika aligonga mrango na ulikuja kufunguliwa na aliefungua alikuwa ni binti.
"Brey huyu ni nani uliemleta hapa alafu mbona umemfunga kamba pia nini kimekufanya uumie kama hivyo.!?"
Yule mwanamke alikuwa na maswali mengi ya kumuuliza Brey lakini Brey hakutaka kumjibu zaidi ya kumuomba aondoke.
"Lakini Brey jamani mbona....!!"
"Hey Lissa nimesema nenda sahizi nina kazi kubwa sana nataka kumalizana na huyu mwanamke kwahiyo nakuomba uende haraka sina muda wa kupoteza hapa"
Brey alizungumza kwa kufoka na kumfanya Lissa atii kile alichoambiwa.
Lissa alikuwa ni binti ambae yupo kwenye mahusiano na Brey yapata week sasa lakini kwa kitendo cha kufukuzwa usiku huo alafu akiangalia Brey alifika hapo na mwanamke basi alijihisi wivu sana na roho kumuuma.
Basi alichukua kila kilicho chake na kutoka nnje lakini alipotoka alitoa simu yake na kupiga mahali.
"Jamani natumai hapo ni kituo cha polisi, sasa nilikuwa nataka kuripoti kuhusu mtuhumiwa mliekuwa mnamtafuta kwa zaidi ya week, mtuhumiwa ambae alilipua bomu uwanja wa ndege kwahiyo nitawapa location alipo na namba ya mtaa ili mfike haraka na kumshika"
Lissa baada ya kutoa hayo maelekezo kwa polisi alijikuta akitabasamu maana kwa kiasi kikubwa alikuwa amemkomesha Brey hivyo alichofanya ni kutuma information zote kwa polisi na kuondoka zake akisubiri majibu.....ITAENDELEA....
- Unafikiri nini kitafuata hapo..je Brey atashikwa na polisi na kwanini simulizi iitwe Penzi La Mtekaji..!?
Basi nikwambie huu ni mwanzo tu wa simulizi yetu bomba lakini nikusihi tukutane sehemu ya pili ya mkasa huu wa kusisimua..
Sehemu ya Pili soma hapa