Kasomi
JT Founder
Firefox imefuata hatua za browser ya Safari ya Apple - kwa kuanza kuweka mfumo wa kuzuia na kuficha IP (anuani) ya mtumiaji akiwa anaperuzi mtandaoni.
Mfumo huo wa Firefox utaitwa Firefox VPN na browser ya Firefox itakuwa inasafirisha taarifa ambazo mtu anaperuzi katika seva za VPN na kuweka ugumu kwa website ambayo umeifungua kuona IP yako, taarifa zako na mahali ulipo.
Pia mfumo huo utazuia (ISP) kama vile mitandao ya simu na internet provider wako kuona website ambazo umefungua na activities zako za mtandao.
Mfumo huu unafanana na Private Relay ya Apple ambayo ipo katika browser ya Safari.
Mozilla imesema huduma hii itakuwa ni bure kabisa na speed yake itakuwa sawa na zaidi ya speed ya kawaida. Mozilla imesema lengo ni kuficha data za mtumiaji na sio kutoa huduma za VPN hivyo mtu hataweza kubadili location ya VPN. Hata Safari pia inaweza kufanya hivyo lakini mtu hawezi kubadilisha general location ila itaficha ile exactly location (precise location).