Advertise here

Paka ahukumiwa kifungo cha nyumbani Nchini Ufaransa

Kasomi

JT Founder
1448

SikiaHii: Paka mmoja nchini Ufaransa amehukumiwa kifungo cha nyumbani baada ya jirani kulalamika kwamba paka huyo alikuwa na tabia ya kurukaruka na kuingia kwenye bustani yake.

Mmiliki wa paka huyo, Dominique Valdes kutoka Agde, pwani ya kusini mwa Ufaransa, amesema tabia ya paka wake aitwaye Remi tayari imemgharimu euro 2,050 kwa faini na fidia kwa jirani yake.

Inaripotiwa kwamba paka huyo amemzuia jirani "asifurahie bustani yake."

Hata hivyo, wapenzi wa paka wana wasiwasi kwamba amri ya mahakama inayomzuia Remi kutoka nje inaweza kufungua njia ya paka wengine kupewa kifungo cha nyumbani.

Chama cha kutetea maslahi ya wanyama cha Ufaransa kimeonya kwamba uamuzi huo unaweza kumaanisha "paka watalazimika kufungwa kwa kamba" ili kuwazuia wasitangatange.

Hivi, paka wa Afrika na walioko Ulaya wako sawa? 🤔
 
Back
Top