Advertise here

Chuma cha Chuma ahukumiwa miaka 3 na fainiya silingi 500,000

Kasomi

JT Founder
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Ferdnand Ndikuriyo (27) maarufu kama Chuma cha Chuma’, ambaye ni raia wa Burundi, kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Shilingi 500,000 baada ya kukutwa na hatia ya kuishi nchini Tanzania bila kibali, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
1738789263923.jpg

Hukumu hiyo imetolewa leo, Februari 5, 2025, na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa.

Ndikuriyo, ambaye ni msanii maarufu wa muziki, alikamatwa kwa kosa hilo Septemba 18, 2024, katika eneo la Las Vegas Casino, Upanga wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam.

Hakimu Ruboroga alisema kuwa mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya pili na kwamba anahitaji kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo kama hivyo.

Chanzo : Clouds media
 
Back
Top