john achila mukumwa
Member
Dhambi ni tamu. Tupate habari zaidi
Dhambi ni Nini?
Dhambi ni tendo, hisia, au wazo lolote linalopingana na viwango vya Mungu. Inatia ndani kuvunja sheria za Mungu kwa kutenda mabaya, au ukosefu wa uadilifu, kwa maoni ya Mungu. (1Yohana 3:4; 5:17). Biblia pia inaeleza kuhusu dhambi ya kutofanya lililo sawa ingawa mtu anajua alipaswa kulifanya (Yakobo 4:17).
Kwa kuwa Mungu ndiye Muumba, ana haki ya kuwawekea wanadamu viwango (Ufunuo 4:11), tunawajibika kwake kwa matendo yetu (Warumi 14:12).
Dhambi zote ni sawa. Dhambi vile vile humhukumu mwenye dhambi, kwa sababu hata dhambi ndogo kabisa ni onyesho la uasi dhidi ya Mungu. Tunapowasaidia wanafunzi kuelewa dhambi ni nini hasa, basi tumewasaidia kuelewa kwamba dhambi, kiini chake, ni uasi dhidi ya wema mkuu wa Mungu.
Dhambi ni kuvunja sheria za Mungu. Imeandikwa, katika 1Yohana 3:4: "kila atendaye dhambi afanya uasi." Kitabu cha 1Yohana 5:17 kinasema "kila lisilo la haki ni dhambi na dhambi iko isiyo ya mauti."
Je amri za Mungu ni zipi?
Mungu aliziandika na kwa vidole vyake mwenyewe kwenye mawe (Kutoka 20:2-17):
"1 Mimi ni Bwana Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
2 Usijifanyie sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho chini majini, chini ya dunia usivisujudie wala kuvitumikia kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wako ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.
3 Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
4 Uikumbuke siku ya sabato, uitakase, siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, maana siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba, kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya saba, akaitakasa.
5 Waheshimu baba yako na mama yako sikui zako zipate kuwa nyingi katika nchi uliyopewa na Bwana Mungu wako.
6 Usiue. 7 Usizini. 8 Usiibe. 9 Usimshuhudie jirani yako uongo.
10 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako."
Sheria za Mungu zimefungwa kwa fungo moja: "Upendo". Imeandikwa, Mathayo 22:37-40: "Mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote". Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo. Nayo ni hii: "mpende jirani yako kama nafsi yako".
Je, kuna dhambi fulani ni mbaya zaidi kuliko nyingine?
Ndiyo. Kwa mfano, Biblia inasema kwamba watu wa Sodoma walikuwa “wabaya”, nao walikuwa wakitenda dhambi “nzito sana” (Mwanzo 13:13; 18:20).
Tambua mambo matatu yanayoamua uzito wa dhambi.
Ubaya: Biblia inatuonya tuepuke dhambi nzito kama vile uasherati, kuabudu sanamu, wizi, ulevi, unyang’anyi, uuaji, na kuwasiliana na pepo (Ufunuo 21:8; 1Wakorintho 6:9-11).
Biblia inatofautisha dhambi hizo na dhambi zinazofanywa bila kukusudia, kama vile, maneno au matendo yanayowaumiza wengine (Methali 12:18; Waefeso 4:31-32). Hata hivyo, Biblia inatusihi tusipuuze dhambi yoyote, kwa kuwa zinaweza kutufanya tutende dhambi nzito zaidi (Mathayo 5:27-28).
Nia: Dhambi nyingine hufanywa kwa kuwa mtu hajui matakwa ya Mungu (Matendo 17:30; 1Timotheo 1:13). Ingawa Biblia haipuuzi dhambi hizo, inazitofautisha na kuvunja sheria ya Mungu kimakusudi (Hesabu 15:30-31). Dhambi zinazofanywa kimakusudi zinatokana na ‘moyo mbaya’ (Yeremia 16:12).
Kurudia kutenda dhambi: Biblia inatofautisha kati ya kufanya dhambi mara moja na mazoea ya kufanya dhambi kwa muda mrefu (1Yohana 3:4-8). Wale walio na ‘mazoea ya kutenda dhambi kimakusudi,’ hata baada ya kujifunza jinsi ya kufanya jambo linalofaa, hupokea hukumu kali kutoka kwa Mungu, kwani huonesha dharau (Waebrania 10:26-27).
Wale walio na hatia ya kutenda dhambi nzito, wanaweza kulemewa na uzito wa makosa yao. Kwa mfano, Mfalme Daudi aliandika hivi: “Makosa yangu yamepita juu ya kichwa changu; kama mzigo mzito, ni mazito sana kwangu” (Zaburi 38:4).
DHAMBI NI TAMU
Dhambi ni tamu. Unapoitenda ni tamu, lakini mwisho wake ni majuto.
Hebu tuangalie Methali 20:17: “chakula kipatikanacho kwa hila ni kitamu kwa mtu, lakini baadaye kinywa chake kitajazwa changarawe” (kama vile dhambi inaweza kuwa tamu mwanzoni, lakini baadaye matokeo yake huleta kukata tamaa).
Dhambi ni tamu sana pale unapoifanya au kuiwaza muda huo.
Dhambi ina ladha tamu, lakini inageuka kuwa chungu ndani ya matumbo yetu.
Utakatifu mara nyingi huonja uchungu, lakini hubadilika kuwa tamu ndani ya matumbo yetu.
Dhambi ni tamu lakini ni sumu inayoua roho na mwili na mwisho wake ni mauti ya milele.
JE, INAWEZEKANA KUEPUKA KABISA KUTENDA DHAMBI?
Hapana. Biblia inasema kwamba “wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23, 1Wafalme 8:46; Mhubiri 7:20; 1Yohana 1:8).
Kwa nini? Mwanzoni, wanadamu wawili wa kwanza, Adamu na Hawa, hawakuwa na dhambi.
Ni kwa sababu waliumbwa wakiwa wakamilifu, kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27).
Hata hivyo, walipoteza ukamilifu wao walipomuasi Mungu (Mwanzo 3:5-6, 17-19).
Kisha, walipozaa watoto, waliwapitishia dhambi ya kutokuwa wakamilifu (Warumi 5:12).
Mfalme Daudi wa Israeli alisema, “nilizaliwa kwa maumivu nikiwa na kosa” (Zaburi 51:5).
KAMA DHAMBI NI TAMU, TUTAPONAJE?
Biblia inatoa tumaini kupitia Isaya 55:7:
"Mtu mbaya na aache njia yake,
Na mtu asiye haki aache mawazo yake;
Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu;
Na arejee kwa Mungu wetu,
Naye atamsamehe kabisa".
Hivyo, dhambi ni tamu, lakini, Mungu ni mwingi wa rehema (Waefeso 2:4-5).
Ametoa tumaini la kusamehe.
Muumini atumie tumaini hilo kwa kufanya yafuatayo:
1. Kukubali kuwa ametenda kosa
2. Kutubu mbele za Mungu
3. Kumwomba Mungu rehema/msamaha
4. Kushika na kutekeleza Neno la Mungu bila kuchoka
5. Kutorudia kutenda dhambi