Advertise here

Je ni sahihi kula damu au nyama mbichi?

Je ni sahihi kula damu au nyama mbichi?

Kwa asili, ulaji wa nyama mbichi ni hatari kwa afya ya mwili, kwani nyama mbichi ina minyoo na wadudu wengi wasiionekana kwa macho
, ambao ni hatari kwa afya na tumepewa maagizo ya kuitunza hii miili, lakini nyama iliyopikwa inakuwa salama kwani inaua vimelea hivyo.

Pia, ulaji wa nyama mbichi unaweza kuashiria uwepo wa roho nyingine ndani ya mtu, na mara nyingi roho ya ukatili inawaingia watu walao nyama mbichi.
Maandiko yanavyosema kuhusu kula damu au nyama mbichi.

AGANO LA KALE
Mwanzo 9:4-5:

4 Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile. 5 Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.

Kutoka 12:8-9:
Wakati wana wa Israeli wanatolewa Misri, ule usiku Bwana MUNGU aliwaambia waile pasaka, ambapo waliagizwa wamtwae mwanakondoo na kumuoka motoni, wamle pamoja na mboga chungu lakini wasimle mbichi.
Kutoka 12: 8 “Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu. 9 MSIILE MBICHI, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani”.

Mambo ya Walawi 13:15:
Kuhani ataiangalia hiyo nyama mbichi, naye atasema kuwa yu najisi; ile nyama mbichi ni najisi; ni ukoma.

Mambo ya Walawi 17:10-11:
10 Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake.
11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.

Mambo ya Walawi 19:26:
Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.

Kumbukumbu la Torati 12:16:
Lakini msiile damu; imwageni juu ya nchi kama maji.

AGANO JIPYA

Marufuku ya kula damu imethibitishwa katika Agano Jipya

Matendo 15:28-29:
Yeyote anayeamini kwamba katazo la Agano la Kale juu ya damu limefutwa na injili, anaweza kusoma jinsi Baraza la Mitume huko Yerusalemu (50 BK) lilivyoamua juu ya hili. Mtume Yakobo, mwenyekiti wa baraza hili, alitangaza katika hotuba yake ya kumalizia uamuzi wa umoja wa kutaniko, ambao Roho Mtakatifu alikuwa ameuleta. Alisema: 28 “Kwa maana inampendeza Roho Mtakatifu na sisi kutokulemea zaidi ya hayo yaliyo lazima, 29 yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na vilivyosongolewa, na uasherati. Mkijiepusha nayo, mwafanya mema. Wasalamu".

Tafsiri nyingine kuhusu sehemu hii ni kama ifuatavyo:
"Roho Mtakatifu na sisi tumeamua kwamba hatutaweka mzigo wowote juu yenu zaidi ya mambo haya ya lazima-kwamba msiwe na uhusiano wowote na nyama ambayo ilikuwa sehemu ya dhabihu ya sanamu, kwamba msile nyama ya wanyama, ambayo haikutolewa kabisa kwa damu ilifumbwa."

Mtu hapaswi kupuuza ukweli kwamba uamuzi huu ulikuja chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu baada ya kifo cha Yesu msalabani na kufufuka kwake. Taarifa hii ya kibiblia inaunga mkono maoni kwamba kanuni za Agano la Kale juu ya afya bado zinatumika leo. Hawakusulubishwa msalabani au kukomeshwa kama sheria ya sherehe, ambayo ilielekeza kwa Yesu na huduma yake ya ukombozi kupitia ishara.

Matendo ya Mitume 15:20:
"bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu".

Mathayo 27:24-25:
24 “Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe. 25 Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu”. Pilato alinawa kwa vile alijua kuwa kwenye damu ndipo kuna uhai.

KWA UJUMLA

KIMWILI
Kwa asili, ulaji wa nyama mbichi ni hatari kwa afya ya mwili, kwani nyama mbichi inaweza kuwa na minyoo na wadudu wengi wasiionekana kwa macho.
Ulaji wa nyama mbichi unaweza kuashiria uwepo wa roho nyingine ndani ya mtu, na mara nyingi roho ya ukatili inawaingia watu walao nyama mbichi.

KIROHO
Atakayekula damu au nyama mbichi, ya aina yo yote, Mungu atakunja uso wake juu ya mtu huyo alaye damu, na Atamkatilia mbali yeye na watu wake. Hiyo ni kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu. Kula damu ni chukizo kwa Mungu, maana yake ni kwamba hairuhusiwi. Hivyo, siyo sahihi kula damu wala nyama mbichi.

Biblia inasisitiza kuwa mtu asile nyama pamoja na uhai wake, yaani damu, kwa maana mtu anapokula damu, Mungu ataukata uhai huo mikononi mwake yeye aliyekula.

Kuna baadhi ya watu nchini, wanakula na kunywa damu mbichi au iliyochemshwa. Kama tulivyoona, damu ni uhai, hivyo, unapokunywa au kula damu, maana yake ni kuwa unakula uhai wa kiumbe hicho, jambo ambalo Mungu mwenyewe amelikataza na kuonya kupitia Neno Lake.
 
Back
Top