Advertise here

Ethan Zuckerman Mgunduzi wa Pop-up ads Mtandaoni

Kasomi

JT Founder
1764962752336 (1).jpg

Miaka ya 1990, intaneti ilikuwa bado changa, tovuti zilikuwa chache, na biashara mtandaoni ndiyo ilikuwa inaanza. Katika kipindi hicho, kijana mhandisi aitwaye Ethan Zuckerman alifanya kazi Tripod.com, moja ya majukwaa ya mwanzo yaliyowawezesha watu kutengeneza kurasa zao binafsi mtandaoni. Hakujua kwamba kazi yake ndogo angeifanya kuwa sehemu ya historia inayosumbua hadi leo.

Tripod ilitegemea matangazo ili kupata mapato. Lakini kulikuwa na tatizo: baadhi ya makampuni ya matangazo hayakupenda nembo zao kuonekana karibu na maudhui ya watumiaji ambayo wakati mwingine yalikuwa yasiyoendana na maadili yao. Hivyo, walihitaji njia ya kuonyesha tangazo bila kuligandisha kwenye ukurasa wenyewe.

Ndipo Zuckerman akaandika kipande kidogo tu cha kodi, ambacho kingeonyesha tangazo la ghafla linaloruka juu ya ukurasa, njia aliyodhani ilikuwa safi, isiyoingilia maudhui ya mtumiaji, na ingewaridhisha watangazaji. Hakukusudia kukera mtu… aliunda tu suluhisho la muda.

Lakini kadri intaneti ilivyokua, suluhisho lake likawa zana kubwa ya matangazo mtandaoni. Pop-up ads zikaanza kuonekana kila mahali, zikiruka ghafla, zikivuruga matumizi, na mara nyingi zikifunga hata kurasa nzima. Wavuti nyingi zikalikumbatia wazo hilo kwa kasi, na mwishowe likawa moja ya mambo yanayochukizwa zaidi na watumiaji wa intaneti duniani.

Miaka mingi baadaye, Zuckerman alikiri hadharani kuwa hakuwa na wazo kwamba mawazo yake yangesababisha kero kubwa kiasi hicho. Katika makala yake ya mwaka 2014, aliandika kwa uaminifu:
“Kama kuna mtu wa kulaumiwa kwa kuanzishwa kwa pop-up ads, huyo ni mimi. Na niseme tu… samahani sana.”

Leo, Zuckerman ni mtafiti na mhadhiri maarufu anayepinga mifumo ya matangazo ya mtandaoni ambayo inawafuata watumiaji, na mara nyingi anapendekeza suluhisho salama na la kibinadamu zaidi katika teknolojia.

Kutoka wazo dogo la mhandisi mmoja, hadi kuwa tabia iliyobadilisha jinsi tunavyotumia mtandao, hii ndiyo safari ya Ethan Zuckerman, mgunduzi asiyejivunis matangazo ya ghafla.
 
Back
Top