Øffïçïäl Dülly Tz
New member
Story.........PENZI LA MTEKAJI
Present.....Simulizi Za Dully
Mtunzi.....Official Dully Tz
WhatsApp...0628924768
Mkasa..wa..kusisimua
Sehemu..Ya..{02}
(Seaeon two)
ILIPOISHIA.....
"Jamani natumai hapo ni kituo cha polisi, sasa nilikuwa nataka kuripoti kuhusu mtuhumiwa mliekuwa mnamtafuta kwa zaidi ya week, mtuhumiwa ambae alilipua bomu uwanja wa ndege kwahiyo nitawapa location alipo na namba ya mtaa ili mfike haraka na kumshika"
Lissa baada ya kutoa hayo maelekezo kwa polisi alijikuta akitabasamu maana kwa kiasi kikubwa alikuwa amemkomesha Brey hivyo alichofanya ni kutuma information zote kwa polisi na kuondoka zake akisubiri majibu.....ENDELEA....
Polisi baada ya kupata onformation kutoka kwa Lissa hawakutaka kulaza damu walichukuzana majeshi na majeshi ili kwenda kumnasa Brey pia walikuwa na tahadhari kubwa sana maana wanaekwenda kumnasa ni mtu hatari sana na inasadikika alilipua bomu uwanja wa ndege siku chache zilizopita.
"Jamani kama ambavyo nimewaambia kuwa tunaekwenda kumshika ni mtu hatari sana, hatujui yupoje wala anaonekana vipi lakini ni mtu hatari hivyo tunatakiwa tuwe na tahadhari kubwa sana la sivyo tutajikuta wote tunaangamia"
Alizungumza askari mkuu wa kikosi ambae alikuwa akiwapa tahadhari kubwa vijana wake juu ya kwenda kumnasa Brey.
"Lakini afande nilikuwa nataka kuuliza kitu, ni sawa unavyosema kwamba tuwe makini lakini nataka kufahamu tunaekwenda kumshika ni sahihi isije kuwa tunaekwenda kumshika sio kwasababu mlipuaji bomu hatujamuona hata sura.!?"
"Ni swali zuri lakini usijali acha tukamnase huyo mtu kama atakuwa sio yeye tutajua tu wakati wa kumuhoji kwahiyo hatuna time ya kuchelewa, jipakieni kwenye magari safari ianze"
Basi baada ya amri kutolewa na kamanda wa kikosi ilibidi polisi wote waingie kwenye magari na safari ilianza kuelekea mahali ambapo walipatiwa maelekezo.
Huku kwa Brey baada ya kumfukuza Lissa na kuingia ndani alimtaka Karina atulie kwenye sofa huku bado akiwa na kamba zake mikononi kisha alielekea kwenye chumba chake na baada ya muda alirudi akiwa na sanduku la huduma ya kwanza.
Aliketi kwenye sofa linalofuata na kuanza kujifanyia huduma ya kwanza lakini kwa upande fulani alikuwa akihangaika maana majeraha aliyokuwa nayo ilikuwa ni mguuni na mgongomi hivyo upande wa mgongoni ilikuwa shida kujitibu.
"Samahani naweza kukusaidia.?"
Sauti hiyo ilisikika na kumfanya Brey ageuke na aliekuwa akihitaji kumpa masaada alikuwa ni Karina, mwanamke ambae alimteka.
"Hapana nitaweza kufanya mwenyewe.
Brey hakutaka msaada wa karina aliendelea kujifanyia huduma mwenyewe lakini Karina aliinuka na kimsogelea Brey kisha aliketi nyuma yake na kuchukua vifaa husika kisha alianza kumpatia huduma ya kwanza.
"Usijali mimi ni mwanafunzi katika chuo cha kusomea udaktari kwahiyo majeraha kama haya madogo madogo nafahamu jinsi ya kuyatibu hivyo nakuomba uwe mpole"
Karina alizungumza kwa ujasiri na kumfanya Brey amuamini lakini Karina alikuwa na jambo lake ambalo alilipanga kichwani bila Brey kufahamu.
Wakati karina akiendelea kumpa huduma ya kwanza Brey kuna dawa aliichukua ya usingizi na kuichanganya kwenye dawa ya ganzi kisha alimtaka Brey ajichome ili atakapomfanyia huduma basi asiweze kuhisi maumivu.
Brey aliipokea bila kufikiria alijichoma na hapo sasa Karina akaona tayari amefanikiwa mpango wake.
Alimpatia huduma vizuri na baada ya kumaliza alifunga jeraha kwa bandage kisha Brey aliinuka na kuelekea jikoni ambapo baada ya dakika kama mbili alirejea akiwa na pakti mbili za biscuit.
"Najua upo na njaa sana lakini kamata hii itapoza njaa yako na utajisikia poa sana"
Brey alimrushia patki moja Karina ambae aliipokea lakini hakutaka kuifungua alikuwa akimtazama Brey akisubiri majibu ya ile dawa aliyomchoma.
"Samahani kakaangu mbona unanijali kiasi hiki una malengo gani na mimi kama huna shida na mimi si uniache tu niende na harakati zangu.!?"
"Sitaki maswali yasiyo na kichwa wala miguu kwani unafikiri ukiwa umehukumiwa kunyongwa si unaulizwa unataka nini ili upatiwe kabla ya kifo chako, kwahiyo tulia wewe ni pesa ndio maana nakujali sana"
"Ok sawa"
Karina ilibidi akubali maana alijua muda wowote kutoka hao lazima Brey atalala na yeye atapata nafasi ya kutoroka lakini ghafla sauti za magari ya polisi zilianza kusikika nnje kuashiria tayari serikali imefika.
Hofu ilimtanda ghafla Brey lakini alipomtazama Karina alimuona akiwa hana wasiwasi ndio kwanza alikuwa akitabasamu.
"Wewe mshenzi ndiye umeita polisi eeh sasa nakuuwa.!!"
"Jamani mimi sifahamu kitu kwanza simu hiyo nimetolea wapi wakati muda wote umenishikilia au huenda yule mwanamke wako amekuuza lakini mimi sijui chochote na wala sijaita polisi"
Maneno ya Karina yalimfanya Brey atambue huenda ni kweli yule mwanamke amemuuza lakini hakutaka kuliwazia sana jambo hilo ila alichowaza ni kumchukua Karina ili waondoke.
"Hebu nifuate tafadhali"
Brey alizungumza huku akiinuka lakini alijikuta nguvu zikimuisha na kurudi tena chini yaani alikuwa ni kama mtu aliekunywa pombe kali iliyomlewesha.
"Wewe mwanamke umanifanyie nini.!?"
"Mimi sijui lakini nikwambie tu kwaheri ila siku nyingine usimuamini mtu yeyote kwenye maisha yako"
Karina alimaliza kuzungumza hayo na kuinuka kwenda kufungua mrango ambapo alikutana na jeshi kubwa la polisi likiwa limetanda nnje.
"Upo chini ya ulinzi hutakiwi kupiga hatua yeyote na mikono weka nyuma ya kichwa"
Polisi walitoa amri lakini Karina alijitetea kwamba ahusiki na chochote ila muhusika mkuu yupo ndani.
Kweli polisi walipomtazama vizuri Karina walimtambua ni binti wa Mr Mbega maana walikuwa kwenye oparesion ya kumtafuta hivyo walimchukua na kumuwekea usalama kisha baadhi ya polisi waliingia ndani na kutoka wakiwa na Brey ambae alikuwa hajitambui na kwa mbali sana alimuona Karina akimtazama.
Alikuwa hana ujanja tena na hata ile mask yake usoni alikuwa ametolewa hivyo ikawa rahisi kwa Karina kumuona vizuri Brey na kushangaa maana alikuwa ni kijana mdogo sana wa makamo yake au huenda amezidiwa mwaka mmoja.
**************
Basi muda huo huo waandishi wa habari nao walifika na kuanza kurusha tukio live lakini upande wa mama Karina alikuwa busy ameketi sebuleni na mawazo mengi yakiwa yamemuandama kuhusu binti yake ambae ndiye alikuwa kitinda mimba wake.
"Mama hebu tazama hizi taarifa huyu si Karina anaonekana kwenye television au sio yeye.!?"
Alikuwa ni dada wa kazi alizungumza kumwambia bosi wake huku akiwa mwenye furaha sana na hata mama Karina alipotazama na kuthibitisha alikuwa ni binti yake basi alinyoosha mikono na kushukuru.
"Oh jamani binti yangu nashukuru sana amepatikana na yupo mzima lakini kwanini mume wangu hapokei simu jamani.!?"
Mama Karina alijaribu kuchukua tena simu na kumpigia mume wake lakini simu ilikuwa ikiita pasi na kupokelewa, hakuchoka alipiga tena na tena.
Lakini wakati yeye anapiga simu huku mume wake na kijana wake walikuwa nnjiani na kwa bahati mbaya gari ilikuwa imewaharibika hivyo walikuwa wamesimama hapo kwa muda na kuangalia shida ni nini.
"Lakini baba mbona unashindwa kupokea simu ya mama labda anataka kukwambia jambo la maana alafu wewe unapuuzia.!!"
Godwin ambae ni mtoto wa Mr Mbega alizungumza huku akitoa simu ndani ya gari na kumpatia baba yake.
"Ah huyu hana jipya ila anataka kunipa lawama tu!"
Mr Mbega aliipokea kwa manung'uniko lakini kitendo cha kuweka sikioni alimsikia mke wake akiongea kwa furaha na kumtaarifu juu ya kupatikana kwa Karina.
"Unasema kweli Karina amepatikana oh asante Mungu basi tunarudi sasahivi maana gari imetuharibikia njiani kwahiyo tunarekebisha haraka sasahivi tunarudi"
Mr Mbega alikata simu akiwa na furaha sana na hata alipomtaarifu kijana wake walijikuta wakifurahi kwa pamoja.
Wakati wapo na nyuso za furaha mara simu ya Mr Mbega ilianza kuita na waliokuwa wanapiga walikuwa ni wale watekaji hivyo alipokea akiwa mwenye kujiamini sasa na aliongea alivyotaka yeye.
"Jamani hebu kwanza msinipelekeshe kama vipi huyo mtoto mchukueni awe wa kwenu sina shida na mtoto tena au ikiwezekana mumuuwe basi"
"Unajua mzee sisi tupo serious alafu bunti yako......"
Kabla kauli hiyo haijamalizwa Mr Mbega alikata simu na kuzima kabisa, kitendo kilichopelekea wale watekaji kuchukia sana maana walijua tayari deal lao limeota mbawa na pesa waliyoitarajia hawatoipata tena.
"Yaani huyu mpuuzi huyu amefanya tukose mamilion ya pesa kijinga daaha kwakweli sitamuacha salama lazima nimtafute nimmalize kabisa"
"Ni sawa lakini chanzo ni wewe mwenyewe yaani kabla pesa haijafika umeanza kumzingua yule dogo sasa hatimae mambo yamekuwa hivi alafu unaanza kusema pesa umekosa kwasababu yake wakati wewe ndiye sababu"
Basi zilikuwa ni lawama tu za watekaji hao lakini huku upande wa binti ambae amemuuza Brey yaani upande wa Lissa mambo yalikuwa mazuri tu na wakati huo alikuwa nyumbani kwake na mwanaume mmoja mtu mzima na huyo ndiye alikuwa mpenzi wake ila kwa Brey alitumwa kwa sababu maalum.
"Sasa nafurahi sana Lissa mpenzi kwa kazi nzuri uliyofanya, hapa polisi lazima watatambua Brey ndiye amelipua uwanja wa ndege"
"Yah alafu sasa ushahidi nimeuweka wazi tu kwahiyo kama ameshikwa lazima nyumba yake ikaguliwe na kama itakaguliwa na kukuta mabaki ya mabomu yaliyolipuliwa uwanja wa ndege basi lazima akaozee jela hahaha"
Ilikuwa ni furaha sana kwa wawili hao maana kesi tayari walikuwa wameiuza kwa mtu mwingine na walifanya hivyo kwasababu walikuwa na chuki juu ya Brey hasa baada ya kutemana na mzee huyo ambae zamani alikuwa akimmiliki Brey kwenye majukumu yake.
"Yaani hawa ni watoto wadogo tu wameanza kazi hizi juzi kwahiyo acha tuwafunze adabu na lazima atakwenda kufia jela hahaha"
Basi mambo yalikuwa ni kama hivyo na walichokipanga kilikuwa kimetimia ila msala ulibaki kwa Brey ambae alikuwa ameshikiliwa na polisi akiwa hajui hatima yake.
**************
Uchunguzi ulifanyika na baada ya kunasa ushahidi ndani ya nyumba ya Brey walimvisha pingu na kumpakia kwenye gari kisha safari ilianza kuelekea kituoni na wakati huo Brey alikuwa hajitambui maana dawa aliyochomwa na Karina ilikuwa imemlalisha kabisa.
Safari ilianza kuelekea kituoni lakini wakiwa njiani Brey alianza kurejewa na fahamu taratibu sana ila alipotazama pembeni yake kulikuwa na polisi ambao walimzunguka pia mikononi mwake kukiwa na pingu ambayo ilifanya mikono yake kuto kuwa na uhuru.
Alitulia kama dakika mbili kujitambua baada ya kutoka kwenye usingizi mzito na mwisho mdipo akili ya kutoroka mikononi mwa hao polisi ilimjia.
Hakutaka kuchelewa alipeleka mikono yake upande wa dereva na kumpiga kabali maana yeye alikuwa kwenye siti za nyuma hivyo ikawa rahisi kukamata shingo ya dereva.
Kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana na kushangaza kwa polisi hao lakini bahati mbaya walikuwa wakipita katika mlima hivyo kwenye purukushani za askari kumtoa Brey asiendelee kumkaba dereva zilipelekea gari hiyo kupinduka na kuangukia bondeni maana hata dereva alikosa balance kabisa ya kuzuia gari.
Ilikuwa ni ajali mbaya sana iliyotokea hapo na mpaka gari ilipofika chini ilikuwa tayari imeharibika vibaya mno huku askari baadhi wakiwa wamepoteza fahamu ila mmoja alikuwa bado na fahamu zake lakini alikuwa amebanwa hivyo alishindwa kujitoa hapo.
Kwa upande wa Brey nae hakupoteza fahamu ila alikuwa ameumia vibaya sana hivyo alijitoa kwenye gari hiyo, alichukua funguo kwa askari mmoja na kujifungua pingu kisha alitokomea pasipo julikana huku hali yake ikiwa mbaya sana.
Upande wa Mr Mbega na kijana wake alikuwa na furaha sana baada ya Karina kupatikana hivyo walikarabati haraka gari yao na ilipowaka walipanda ili kuondoka lakini kabla Mr Mbega hajakanyaga mafuta alitazama kwenye site mirror ya kuangalia nyuma na kumuona mtu ambae alimuacha na mshangao sana.
"Baba unashangaa nini hebu twende gari tayari imewaka unajua muda umeenda sana.!"
Godwin alizungumza kumwanbia baba yake ambae bado alikuwa ameduwaa kutazama nyuma hivyo ilbidi nae atazame lakini walichokiona kiliwashangaza sana.
Walimuona mtu akija kwa mwendo wa kuyumba huku mwili wake ukiwa na majeraha mengi yaliyokuwa yakivuja damu hivyo Mr Mbega alipomtazama vizuri yule mtu alimuona akiomba msaada ila bado hawakumtambua alikuwa ni nani na ni nini kimemfanya aumie kiasi hucho....ITAENDELEA....
- Je unafikiri nini kitafuata hapo, mtu huyo ni nani na Mr Mbega atatoa msaada au laa.
Kwanini simulizi iitwe penzi la mtekaji, mimi sifahamu lakini tukutane sehemu ya tatu kujua nini kitafuata....