Kasomi
JT Founder
HABARI Mtu mmoja anayedaiwa kuwa mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) kampasi ya Mbeya, Tido Kadaga amekutwa amefariki dunia kwenye dimbwi la maji katika mtaa wa Maili tano, Kata ya Iganzo Jijini Mbeya.
Tukio hilo limetokeo leo Februari 17,2026 baada ya baadhi ya mashuhuda na wasamiria wema kuripoti taarifa hiyo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufuatia kuona mwili huo ukielea juu ya dimbwi la maji ambapo askari wa jeshi hilo walifika eneo la tukio na kuuopoa mwili huo na kuupeleka Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kwa uchunguzi zaidi.
Akithibitisha tukio hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya, Malumbo Ngata amesema saa 8 mchana walipokea wito wa uwepo wa mtu anayeelea kwenye dimbwi katika Mtaa wa Maili tano Kata ya Iganzo jijini Mbeya, ambapo walifika na kukuta mwili huo ukielea.
Amesema baada ya kutoa mwili amebainika kuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya aliyetambuliwa kwa jina la Tido Kadaga (20), ambapo mwili umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Chanzo: East Africa TV