Advertise here

TANZIA William Bamaga Mwanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) inadaiwa kuuliwa na Abeli kisa uhusiano wa mapenzi na mdogo wake

Kasomi

JT Founder
HABARI Kijana anayejulikana kwa jina la Abel anadaiwa kumuua mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) aitwaye William Bananga (Pichani) akimtuhumu kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mdogo wake wa kike
1748116751407.jpg

Inaelezwa kuwa jambo hilo lilimkasirisha na kumfanya achukue hatua za kumchoma kisu mwanafunzi huyo na kumsababishia kifo

Kufuatia tukio hilo wananchi wenye hasira wameandamana hadi nyumbani kwa mtuhumiwa na kuvunja vioo vya madirisha, kung’oa miwa na kuharibu baadhi ya vitu ndani ya nyumba hiyo

Wakizungumza na wanahabari baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo wameeleza kuwa kijana huyo aliyemuua mwenzake sio tukio lake la kwanza amekuwa akifanya matukio ya kihalifu ya aina hiyo kwa zaidi ya mara tatu na kinachowafanya kuvamia eneo hilo ni kutokana na mama wa kijana huyo kumtetea kijana wake anapofanya matukio ya aina hiyo

Mwenyekiti wa mtaa wa Mlimani Agness Moshi amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa kitendo cha wananchi kuvamia eneo hilo ikiwemo kutaka kuchoma nyumba sio jambo nzuri la lingekuwa na madhara kwa watu wengi zaidi na amezuia wasiendelee na uharibifu huo

Inaripotiwa kuwa Abel alitoroka muda mfupi baada ya tukio na hadi sasa hajulikani alipo.

-------------
Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) kimethibitisha kwa kutoa taarifa hiyo
IMG-20250526-WA0004.jpg

Chanzo: EastAfricaTV
 
Mapenzi Hisia...

Huyu mwanafunzi wa chuo mbona anamwonekano wa umri wa darasa la tatu au nne..au sisi tulisoma MEMKWA ndio maana hyu tunajiuliza chuo alifikafikaje kwa mwonekano huu wa umri
 
HABARI Kijana anayejulikana kwa jina la Abel anadaiwa kumuua mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) aitwaye William Bananga (Pichani) akimtuhumu kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mdogo wake wa kike
View attachment 1138
Inaelezwa kuwa jambo hilo lilimkasirisha na kumfanya achukue hatua za kumchoma kisu mwanafunzi huyo na kumsababishia kifo

Kufuatia tukio hilo wananchi wenye hasira wameandamana hadi nyumbani kwa mtuhumiwa na kuvunja vioo vya madirisha, kung’oa miwa na kuharibu baadhi ya vitu ndani ya nyumba hiyo

Wakizungumza na wanahabari baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo wameeleza kuwa kijana huyo aliyemuua mwenzake sio tukio lake la kwanza amekuwa akifanya matukio ya kihalifu ya aina hiyo kwa zaidi ya mara tatu na kinachowafanya kuvamia eneo hilo ni kutokana na mama wa kijana huyo kumtetea kijana wake anapofanya matukio ya aina hiyo

Mwenyekiti wa mtaa wa Mlimani Agness Moshi amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa kitendo cha wananchi kuvamia eneo hilo ikiwemo kutaka kuchoma nyumba sio jambo nzuri la lingekuwa na madhara kwa watu wengi zaidi na amezuia wasiendelee na uharibifu huo

Inaripotiwa kuwa Abel alitoroka muda mfupi baada ya tukio na hadi sasa hajulikani alipo.

Chanzo: EastAfricaTV
Katembea nae tu kauwawa je kam angekimbia nae 🏃🏃🏃
 
Back
Top