Raven
New member
Social Media OSINT
Social media OSINT inalenga zaidi kutafuta taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii.
Watu wengi iwe kwa kujua au bila kujua hujikuta wameanika taarifa zao kwenye account zao za mitandao ya kijamii.
Mtandao kama Facebook mtu akifungua account unakuwa unamsumbua na maswali mengi yakimtaka user ajaze taarifa mbalimbali kumhusu kitendo ambacho wengi hujikuta wakotoa taarifa zao na kuziweka hadharani kitendo ambacho kinafanya mtu mwingine azione na kuzipata kwa urahisi.
Taarifa hizo mara nyingi huwa ni taarifa binafsi (kama majina, tarehe ya kuzaliwa, mahali anapoishi, mawasiliano), taarifa kuhusu elimu na kazi anayofanya, vitu anavyopenda (hobbies and interests).
Ikiwa utatumia akili ya kipelelezi kwa chunguza contents za mwenyewe account (user), account anazozifuata, marafiki wa online, content anazoshare, maoni kuhusu mambo fulani, picha/video anazo post(Metadata), muda wa kupost n.k n.k n.k n.k unaweza pata taarifa zaidi kumhusu user (unaempeleleza)
Social Medias ni moja ya sehemu nzuri za kufanyia background check. Nadhani makampuni makubwa pamoja na vyombo vya dola kama (Police) hutumia social media kufanya background check na kupeleleza maisha ya mtandaoni ya watu wanaotaka kuwapa ajira ili kuona kama hawatakuja kuleta noma. (Unaweza jikuta unafanyiwa pyscho analysis au political views zako kama mnapishana unatemwa)
Hapa inabidi uwe mstaarabu tu mtandaoni ili baadae wakianza kukupeleleza isije ikakuletea noma huko baadae.
Account ikiwa Private inakuwa ngumu mtu ambaye hujamfollow kujua unachopost pamoja na taarifa zako zingine. Hivyo ni vizuri kama utaweka account yako private kupunguza kufatiliwa/kupelelezwa na watu wengine.