Advertise here

Kituo cha Runinga cha ITV chashinda Tuzo ya Super brand, Na Azam Media & Bakhressa Group washindi pia

Kasomi

JT Founder
Kituo cha runinga cha ITV kimeshinda tuzo ya Superbrand, ikiwa ni mara ya sita mfululizo kwa kituo hiki kuchukua tuzo hiyo, sababu kubwa ni kutokana na umahiri wake wa kuhabarisha umma.
1677509827771.jpg

Wakati huo nao BAKHRESA GROUP, AZAM MEDIA NI SUPER BRANDS

Kampuni ya Azam Media pamoja na Kampuni mama ya Bakhresa Group zimeng’ara kwenye tuzo za Super Brands (Chaguo la Afrika Mashariki) kwa mwaka 2022 – 2024.

Tuzo hizo zimekabidhiwa kwa kampuni hizo na waandaji wa tuzo hizo katika ofisi za Azam Media zilizopo, Tabata, Dar es Salaam.

Kwa upande wa Azam Media na Bakhresa Group tuzo hizo zilipokelewa na Afisa Uhusiano wa Bakhresa Group, Rehema Salim na Mhariri wa Dawati la Habari na Matukio wa Azam media, Ben Mwang’onda.

Jumla ya kampuni nane zimepokea tuzo hiyo na kukabidhiwa kwao na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrand, Jawad Jaffer.
1677509671547.jpg
 
Back
Top