john achila mukumwa
Member
Unaweza kubatizwa na usipokee Roho Mtakatifu. Unaweza kupokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono au la.
Mambo haya yamekuwa yakiongelewa na baadhi ya watu, bila majibu sahihi.
Hebu tuyaangalie kwa mujibu wa maandiko.
Matendo ya mitume 8, yanasema:
14 “na Mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu,wakawapelekea Petro na Yohana, 15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu, 16 kwa maana bado hawajashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu. 17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu”.
Mambo hayo yanayojadiliwa, yamejikita katika maswali matatu.
1. Je, unaweza kubatizwa na usimpokee Roho Mtakatifu kama hawa wale wa Samaria ilivyokuwa?
2. Je, unaweza mpokea Roho Mtakatifu kwa kuombewa kama Petro na Yohana walivyofanya?
3. Kwa jamii yetu ya kawaida, ni kigezo gani kinatumika kwa mtu kuwabatiza wengine au awe na sifa zipi huyo mbatizaji ili tupate ubatizo sahihi?
Kwanza ni muhimu kufahamu umuhimu wa ubatizo sahihi. Ubatizo sahihi ni kama leseni ya Roho Mtakatifu kukaa ndani ya mtu. Yaani mtu anapobatizwa katika ubatizo sahihi, amemhalalisha Roho Mtakatifu kuingia ndani yake na kuwa wake.
Hivyo Roho Mtakatifu anaweza kushuka juu ya mtu kabla au baada ya kubatizwa. Lakini uhalali wa kukaa moja kwa moja ndani ya mtu unakuja baada ya mtu kubatizwa.
Tuanze na swali la kwanza.
Je, unaweza kubatizwa na usimpokee Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa kwa wale watu wa Samaria?
Jibu ni ndiyo. Kama umeamini na kutubu dhambi zako kwa kudhamiria kuziacha, na ukaenda kubatizwa, lakini hujawahi kusikia lo lote juu ya Roho Mtakatifu, hapo hawezi kuingia ndani yako, kwa sababu Roho hawezi kuja juu ya mtu ambaye hajawahi kabisa kuzisikia habari zake. Ni sharti kwanza mtu huyo ahubiriwe Roho Mtakatifu ni nini, ndipo ashuke juu yake.
Hata Bwana Yesu hawezi kuingia ndani ya moyo wa mtu kama mtu huyo hajahubiriwa kabisa, au hajawahi kusikia kabisa habari za Yesu. Hivyo, kwa mtu aliyeamini na kutubu na kubatizwa ipasavyo, Roho Mtakatifu mwenyewe atahakikisha anamletea mhubiri ambaye atamweleza kuwa kuna kitu kinachoitwa Roho Mtakatifu, ndipo ashuke ndani yake.
Ndicho kilichotokea kwa hawa watu wa Samaria na wale Wakorintho Paulo aliokutana nao.
Soma Matendo 19:
1 “Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; 2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. 7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili”.
Pia, Roho Mtakatifu anaweza kushuka juu ya mtu kabla hajabatizwa, endapo tu atakuwa ameshasikia kuwa kuna kitu kinachoitwa Roho Mtakatifu. Kama mtu ameshasikia kuwa kuna kitu kinaitwa Roho Mtakatifu na jinsi anavyotenda kazi, basi Roho anaweza kushuka juu ya huyo mtu hata kabla hajabatizwa. Lakini ili awe na uhalali wa kukaa ndani ya huyo mtu ni lazima mtu huyo akabatizwe ili kukamilisha wokovu wake.
Ndicho kilichotokea kwa Kornelio akida wa Kirumi wakati Petro amekwenda nyumbani kwake.
Soma Matendo 10:
44 “Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno 45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. 46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, 47 Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? 48 Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha”.
Twende kwenye swali la pili.
Je, unaweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuombewa kama Petro na Yohana walivyofanya?
Jibu ni ndiyo. Unaweza kupokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono, lakini siyo wakati wote.
Mara nyingi watu wanapokea Roho pasipo hata kuwekewa mikono. Mfano ni siku ya Pentekoste. Mitume hawakuwekewa mikono na mtu yeyote. Na hata wakati Petro yupo nyumbani kwa Kornelio kama tulivyosoma hapo juu, watu wale hawakuwekewa mikono na mtu yeyote, lakini Roho alishuka juu yao.
Hivyo, Roho anaweza kushuka juu ya mtu aidha kwa kuwekewa mikono na watiwa mafuta, au bila kuwekewa mikono. Inategemea Roho mwenyewe atakavyopenda. Na pia, jinsi Roho atakavyomuongoza yule mtiwa mafuta anayehudumu.
Tumalizie na swali la tatu.
Kwa jamii yetu ya kawaida ni kigezo gani kinatumika kwa mtu kuwabatiza wengine au awe na sifa zipi huyo mbatizaji ili tupate ubatizo sahihi?
Vigezo vinavyotumika vya mtu kuwabatiza wengine ni vigezo vile vile vya mtu anayetaka kuwa mhubiri.
Mtu akitaka kuwa mhubiri, au mwalimu kwa wengine, ni sharti kwanza awe mwanafunzi wa Kristo. Pili, awe na uwezo wa kufundisha wengine kitu ambacho yeye mwenyewe anakiishi. Na awe na uelewa wa kutosha wa kitu anachokwenda kukifanya. Awe ameitwa na Mungu kweli, na anafahamu kuwa anafanya kazi ya Mungu na si ya mwanadamu.
Kadhalika, mtu anayetakiwa kubatiza wengine anapaswa na yeye mwenyewe kwanza awe amebatizwa katika ubatizo sahihi, na awe na uelewa wa kutosha kuhusu ubatizo. Yaani faida za kubatizwa na hasara za mtu kutokubatizwa, ili aweze kuwafundisha vyema wale ambao watakuja kubatizwa naye. Mtu mwingine ye yote asiyekuwa na vigezo hivyo haruhusiwi kufanya kitendo hicho kitakatifu.