Chozi la DIEGO FRAZAO TORQUATO liliobaki kuwa alama ya Tumaini

Kasomi

JT Founder
Chozi la DIEGO FRAZAO TORQUATO liliobaki kuwa alama ya Tumaini
1671563895974-jpg.338
338

Picha uionayo ni ya kijana mpiga fidla aliyeitwa Diego Frazão Torquato aliyezaliwa mwaka 1997 katika makazi duni ya Para de lucas......Duque de Caxias nje kidogo ya jiji la Rio de Janeiro huko nchini Brazil

Para de Lucas ni makazi duni yaliokithiri maradhi na matendo ya kiuhalifu...hali iliyomuathiri Diego kwa kiasi kikubwa kwani alipofika umri wa miaka 4 alilazwa hospital alikuwa anasumbuliwa na pneumonia na mara kadhaa alikuwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu

Licha ya changamoto zote hizo za maradhi na umasikini lakini bado kijana Diego alikuwa na ndoto za kuwa mpiga fidla (????) na katika imani aliyokuwa nayo aliamini kuwa fidla ndio itakayomtoa kimaisha hivyo aliweka jitihada kubwa sana za kujifunza fidla

Evandro Jeao Silva ...mwanaharakati aliyekuwa anapigania haki za watoto na kuwaepusha na kuangukia kwenye matendo maovu ya kiuhalifu katika maeneo hayo... alikuwa na kikundi Cha muziki ambacho walimkaribisha Diego kuwa miongoni mwao kikundi hicho kikiitwa Afroraggae

Katika hali ya kusikitisha Evandro Jeao Silva aliuliwa na...utajisikiaje ukiwa na ndoto kubwa kisha ukampata mtu sahihi wa kukushika mkono kufikia ndoto zako lakin hata kabla hamjafika hatua moja yule mtu anauawa???

Hicho ndio alichojisikia Diego ...siku ya mazishi wakapanga kupiga fidla ....na hiyo picha ya huyo mtoto mweusi anayetiririkwa na machozi ndio Diego Frazão Torquato....anapiqga fidla huku chozi likimtiririka...anaona Giza limerud tena katika maisha yake...anaona chombo alichopanga kusafiri nacho ili afike nchi ya ahadi KIMEPIGWA DHORUBA WAKIWA MKONDONI. ...ataachaje kulia...machozi yakaanza kama kijito..mto mwishowe yakafanya bahari yalioyomeza ndoto zake

Sikuhiyo Diego alikuwa anaumwa lakini alilazimika kumuaga shujaaa wake

Katika hali ya bahati mbaya zaidi Diego nae alifarikj siku chache baada ya picha hiyo kuchukuliwa na alifariki kwa ugonjwa wa moyo

Katika mazishi ya Diego Frazão Torquay .....bwana Jose Junior alipata kusema hivi " nadhani urithi mkubwa ambao Diego Frazão Torquato ni tumaini na ule utayari wa mabadiliko na kubadilika'

Diego Frazão Torquato alifariki akiwa na miaka 12 tu ila anatambulika katika eneo lake kama alama ya matumaini aliwapa motisha vijana wengi wawe tayari kupigania ndoto zao bila kujali vikwazo vinavyowakabili

Huyo ndio Diego Frazão Torquato na chozi lake lililobaki kuwa alama ya tumaini
 

Attachments

  • 1671563895974.jpg
    1671563895974.jpg
    148.6 KB · Views: 381
Back
Top