Kasomi
JT Founder
HISTORIA YA DIEGO JOTA NYOTA ALIYENG'AA NA KUZIMIKA GHAFLA
Katika viunga vya Massarelos, mjini Porto nchini Ureno, mnamo tarehe 4 Desemba 1996, alizaliwa mvulana aliyepewa jina Diogo José Teixeira da Silva, ambaye baadaye ulimwengu ulimfahamu kwa jina la kisoka Diogo Jota.
Kutoka akiwa mtoto mdogo, Jota aliishi maisha yaliyojaa ndoto na mpira wa miguu.Viatu vyake vya kwanza vya soka vilimpeleka kwenye uwanja wa Gondomar SC, klabu ya mtaa aliokulia. Huko,talanta yake iliibuka kama jua la alfajiri lenye matumaini na mwanga wa kipekee. Hakuwa na kelele nyingi, lakini miguu yake iliimba mashairi mazito ya soka kila alipopiga mpira.
Kipaji chake kilivuka mitaa ya Porto hadi akaingia kwenye mfumo wa klabu ya Paços de Ferreira na ndipo ulipoanza mlolongo wa mafanikio ya kitaaluma. Katika msimu wa 2014/15, akiwa bado kijana, alifanya makubwa na kuwavutia wakongwe wa kandanda.
Mwaka wa 2016, Atlético Madrid walimnasa, lakini kama ilivyo kawaida kwa vipaji changa, Jota alitumwa kwa mkopo huko FC Porto na kisha kwa Wolverhampton Wanderers ambako alijenga jina, akakuwa kipenzi cha mashabiki, akifunga mabao muhimu yaliyowapa matumaini mashabiki wa "Wolves".
Miaka ya 2017 hadi 2020 ilikuwa kipindi cha ufanisi mkubwa. Jota alikuwa mshambuliaji jasiri, mwenye kasi, ujanja na macho ya bao. Alikua mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na mwaka 2020, alifanya uhamisho ulioshtua wengi kwenda Liverpool FC ya Uingereza, chini ya kocha Jürgen Klopp.
Anfield ikawa nyumbani kwake kupya. Jota alichanua akiwa na wachezaji wakubwa kama Mohamed Salah, Sadio Mané na Roberto Firmino. Alifunga mabao ya kihistoria, akaleta ushindani kwenye safu ya ushambuliaji na kuendeleza hadithi ya kijana wa Porto aliyekataa kuota tu bali aliamua kuwa ndoto.
Nje ya uwanja, Jota alijulikana kwa unyenyekevu, mapenzi kwa familia na utulivu wa tabia. Alikuwa mpenzi wa maisha wa mchumba wake wa muda mrefu na hivi karibuni siku tano tu zilizopita walifunga ndoa, wakiahidiana na kuhaidiana maisha marefu yenye furaha na watoto.
Lakini maisha huwa na fumbo kubwa. Leo tarehe 3 Julai 2025, dunia ya kandanda imetetemeka. Diogo Jota amepoteza maisha katika ajali mbaya ya barabarani huko Zamora,Uhispania. Habari ambazo zimekelewa kwa, majonzi na machozi, zikifuta ghafla tabasamu la ndoa yake mpya na kuacha pengo kubwa kwa wapendwa wake na mashabiki duniani kote.
Kwa wengi, alikuwa mchezaji. Kwa wengine, alikuwa shujaa. Kwa familia yake,alikuwa mwana, mume na rafiki. Lakini kwa historia, Diogo Jota atasalia kuwa alama ya azma,bidii na nyota iliyoangaza ghafla, ikazimika ikiwa bado ina mwanga mkali.
Pumzika kwa amani, Diogo Jota.
Tulikuona ukianza kupaa hatukujua ulikuwa njiani kurudi nyumbani mbinguni.