Advertise here

Huyo Mkaka au Mdada unaempenda hebu mwambie huenda nae anakupenda soma hapa

Mtata

Member
Around 2014_2017 nilikuwa nafanya kazi kwenye duka la kuuza nguo huko mbeya.

Sasa mimi kikawaida nilikuwa nafika saa mbili dukani, siku nikiwahi sana nafika saa moja na nusu au nadakika arobaini.

Kikawaida soko lilikuwa linafunguliwa saa 12 asubuhi na kufungwa saa moja usiku. Kuna huyu mdada mmoja tulikuwa tunauza nae kwenye soko moja.

Kila siku nilikuwa nikifika sokoni lazima nimkute amefungua, siku nikikuta hajafungua basi siku hiyo haji kabisa sokoni.

Kuna siku nilikuwa narudi nyumbani jioni ndio nikagundua yule mdada anakaa karibu na ninapokaa mimi, yani kutoka ninapokaa hadi anapokaa yule mdada ni dakika tano tu.

Huyo mdada hatutashinda tukimuita mdada acha tumpe jina tumuite Belema.

Siku moja nilikuwa napita dukani kwake akanambia mbona umechelewa sana, nikamjibu hii ndio mida yangu ya kufika.

Wakati nataka kuondoka nikasema ngoja nijaribu bahati yangu, nikamwambia nipe namba yako uwe unaniamsha asubuhi niwahigi kuamka ili niwe nawahi kama wewe.

Kabla hatujafika mbali kipindi nachukua namba nilikuwa sina hisia nae kabisa nilikuwa namuona kama mshikaji wangu tu.

Akanipa namba, siku inayofuata saa kumi na moja akanipigia simu akasema yeye ndio anajiandaa hivyo na mimi niwe najiandaa anakuja kunipitia twende kazini.

Saa kumi na mbili na dakika kumi hivi akanipigia simu kuwa yupo nje, basi nikamkaribisha ndani akagoma, nilikuwa tayari nimejiandaa hivyo tukaondoka.

Kuanzia siku hiyo ndio ikawa ratiba yetu, asubuhi tunavyoenda kazini na jioni tunvyorudi kazini tulikuwa tupo wote.

Kuna kitu wazungu wanaita kudevelop filling kama sijakosea, huwa inatokea mtu ulikuwa humpendi au unamchukulia rafiki yako lakini ghafla ukaanza kumpenda kimapenzi.

Zile night walk na morning walk zikazalisha hicho kitu, sijui ni kwangu tu au hata kwake. Lakini alikuwa na wivu na mimi, na mimi nilikuwa na wivu na yeye.

Hakuna aliyewahi kumwambia mwenzake anampenda lakini asilimia 99 ya waliokuwa wanatuona pamoja walikuwa wanajua sisi ni wapenzi.

Long story short, Belema alikuja kuolewa na mtu mwingine kabisa, na alinilaumu sana kwamba alionyesha hisia zake kwangu lakini mimi nilishindwa kujiongeza, lakini hata mimi nilimwambia nilionyesha hisia zangu pia lakini yeye alishindwa kujiongeza.

Aliolewa na alihama mkoa, lakini kila mmoja alimpenda mwenzake ila ukimya ndio ulituponza.

Huyo mkaka&mdada unaempenda hebu mwambie huenda nae nakupenda 😁😁.

Akikwambia nilikuwa nakuchukulia kama kaka angu& dada angu mwambie unawajua ndugu zako wote😂😂 huna dada kama yeye.
1736934661878.jpg
 

Attachments

  • 1736934661878.jpg
    1736934661878.jpg
    221.5 KB · Views: 49
Back
Top