Zaa huyo mtoto wewe, Usimsikilize huyo anayesema hayuko tayari kulea

Kasomi

JT Founder
Anaandika Emmanuel Minga

"Her:: Mwalimu Nina mimba ya miez 3 lkn nilipomwambia mwenzang akabadilika anasema nitoe lakini mim naona sio sawa jamani nisaidie ushauri hapa nisije onekana ninakiburi nifanye nini mimi.

Me :: mbona unaujasiri alafu unaogopa? Pole na changamoto hiyo.
Kabla ya kutoa mimba Fikiria hili,

Ni nani mwenye makosa nyie au hichokiumbe mnachotaka kukifanyia ukatili?

Mzazi wako angekufanyia huo ukatili wewe ungekuwepo?

Ona huyo mtoto amekuwa na amekuwa mtu muhimu duniani unafikiri unakuwa umewakosesha watu wangapi fursa ambazo wangezipata kupitia mwanao?

Unajuaje kama huyo mtoto ndiye Angekuwa mkombozi wako wa kesho yako?

Vipi kuhusu kuathirika Kwa mfumo wako wa kizazi, unajua unaweza usipate fursa ya kushika mimba tena?

Huoni unajihatarishia uhai, ukifa utaenda kumwambia huo upumbavu Muumba wako?

Unajua unaweza kujipatia mikosi Kwasababu tu unamwaga damu isiyo na hatia ,sijui kama unalijua hilo!?

Zaa huyo mtoto hujui kesho atakuwa nani? Najua wewe hukumtegemea lakini Mungu alimuandalia nafasi tayari ndio maana akawa nafsi hai.

Watoto wasio tegemewa huwa mara nyingi ndio huwashangaza wazazi wao. Huwenda ndio mtoto aliyebeba muujiza wako, kicheko chako, atakayefuta chozi lako, mtoto wa kutegemewa.

Zaa huyo mtoto wewe. Usimsikilize huyo anayesema hayuko tayari kulea.

Mambo yako hivyo amua wewe hapo, me nitumie Hela yangu ya maziwa namba hiyo hapo".

E.M✍️
 
Back
Top