HIVI NDIVYO WANAVYO FANYA ILI KUHACK ACCOUNT YAKO YA FACEBOOK

Kasomi

JT Founder
HIVI NDIVYO WANAVYO FANYA ILI KUHACK ACCOUNT YAKO YA FACEBOOK
FB_IMG_1738597439222.jpg

Wanaoiba hizi account wanajua kabisa kucheza na akili za wanao watarget. Na wanajua kabisa watu wengi wanapenda pesa za bure hivyo inakuwa rahisi kwao kufanilisha malengo yao.

Sasa leo nataka nikwambie kwa ufupi wanawezaje kufanikisha malengo yao hadi kufikia kukuibia account.

HATUA YA KWANZA.
Kitu cha kwanza wanachokifanya ni kukutamanisha na pesa/fedha ambazo wanadai zinatolewa Taasisi za kifedha, Mashirika ya umoja wa mataifa, watu maarufu au kupitia huduma za mikopo ya kimtandao.
Wakishafanikiwa kukuteka akili basi wanakutumia link ya kuweza kuwasiliana na mtu wanaedai anaweza kukusaidia kupata huo mkopo mara nyongi huwa ni link ya Whatsapp na mara chache saba huwa ni google form link.
Lakini pia huwa wanahakikisha lazima wawasiliane na wewe kupitia namba ambayo umeitumia kujisajiri nayo facebook ili iwe rahisi kukuibia account.
So maswali kama hii namba ndo unayotumia Facebook unaweza kujikuta unaulizwa pale unapo wasiliana nao kupitia mawasiliano waliyokupa.

HATUA YA PILI
Wakisha jiridhisha kuwa namba uliyowasiliana nayo ni ya hiyo ambayo unatumia Facebook basi wanacho kifanya wanaitumia hiyo namba kuingia kwenye account yako na kujaribu kuchange password. Hivyo wanatumia option ya forget password kuweza kuomba kubadirisha passoword. Sasa hatua hii huwa inalindwa na Kitu kinachoitwa Two Factor Authentication ambapo lazima utumie One Time Password (OTP) Ili kuweza kuvuka na kubadirisha password.

Hizi OTP huwa zinatumwa kwenye Namba ambayo umeitumia kujisajiria Facebook.

Sasa ili waweze kuzipata hizi OTP kutoka kwako wanakulaghai kwa kukwambia kuwa wanakuunganisha na huduma ya kuweza kupata hizo Pesa katika mfumo wao au website yao so kuna code zitatumwa kwako na ukiziona basi uwatumie.

Ukiwatumia hizo code wanachokifanya wanaziingiza na kisha kubadirisha password za account yako ya Facebook na kuweka za kwao. Kisha wanabadirisha taarifa zote muhimu ambazo wanajua unaweza kuzitumia ili kurecover account yako.

Na hadi hapi unakuwa tayari umeshapigwa account yako na unakuwa huna uwezo tena wa kuirudisha.

HATUA YA TATU
Baada ya kuichukua account yako wanaanza kuwatumia ujumbe kama waliokutumia wewe watu wako wa karibu ili kuwalaghai na wao waingie kingi kama ulivyo ingia wewe. Na wanafanya hivi wakiamini kuwa huyo mtu hatokuwa na wasiwasi kwani atakuwa anaamini kuwa anawasiliana na wewe na hivyo ataingia kingi tu. Hii inaitwa Impersonation katika ulimwengu wa hacking.

Hadi sasa nina ushahidi wa watu wangu wa karibu zaidi ya 10 ambao wamekumbwa na sekeseke hili na ni mmoja tu ambaye amebahatika kuweza kurudisha accouny yake na aliweza kurudisha kwakuwa aliyemdukua kuna taarifa alisahau kuzibadili na hivyo kufanya iwe rahisi kurudisha hiyo.

USHAURI WANGU KWENU
Kuweni makini sana na watu mnaochat nao hata kama mnawajua. Ukiona mtu anakuletea mchongo wa pesa za bure basi huyo ni wa kumblock na kuachana nae maana yupo kwaajili ya kutaka kukuliza.

Unaweza ona kwenye screenshot mbili hapo chini jamaa alivyokuwa anajaribu kutaka kumuhibia dada hangu Estr Ezekia

Niishie hapa kwa leo

Kwa maswali uliza hapo kwenye comment na usiache kushare na wengine pia waweze kujifunza
 

Similar threads

Back
Top