Kasomi
JT Founder
ASILI YA UDOM - UNIVERSITY OF DODOMA. CHUO KIKUU CHA DODOMA.
Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM kilichojengwa kwenye kilima cha Chimwaga Dodoma Ujenzi wake ulianza hivi.
Aricard Mulokozi ameshiriki Ujenzi huo toka mwanzo. Kabla ya wazo la UDOM wakati wa Utawala wa mfumo wa chama kimoja cha mapinduzi CCM lengo la Ujenzi lilikuwa ni ukumbi wa mikutano ya chama. Na Ujenzi wa ukumbi ulianza mwaka 1990 chini ya ukandarasi wa Korea Kaskazini Kwa kushirikiana na wajenzi wa JKT na JKU.
baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza ndipo ilipobadilishwa likawa jengo la UDOM. Na wakati Ujenzi wa ukumbi unaendelea miaka ya 1990 eneo lote linalozunguka kilima cha Chimwaga lilikuwa pori ambapo leo pametapakaa majengo ya UDOM. Mwanzo katika ramani ya Uendelezaji wa Makao Makuu ya Nchi Dodoma iliyojulikana kwa jina la CDA CAPITAL DEVELOPMT AUTHORITY mipango ilikuwa eneo la Chimwaga yajengwe majengo ya serikali, Bunge pamoja na ukumbi wa mikutano - Chimwaga Complex. Kwa bahati mbaya lengo halikukamilika kwasababu ya pesa. Eneo lllilo na majengo ya UDOM ilikuwa inaanzia Ntyuka hadi barabara kuu ya Dodoma usawa na eneo la Nzuguni. Fedha zilikwamisha mpango mzima maana eneo tu la viwanja vya ukumbi wa Chimwaga Complex uliweza kuwa na egesho la magari yote ya wajumbe ama magari yote ya watumishi wa nchi bila shida. Uamuzi wa kutumia majengo ya ukumbi wa Chimwaga kuwa kianzio cha UDOM ilitokana na ukwasi wa kuendeleza mradi huo. Na kwa busara za alikuwa Raisi wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kufanya majengo ya ukumbi uliokuwa wa CCM kuwa mali ya serikali na hivyo kufanya iwe rahisi kuendeleza eneo hilo. Uratibu wa kujenga UDOM ulianza mwezi March 2007 lakini mpaka chuo kinafunguliwa Septemba 2007 hapakuwa na jengo lolote la UDOM. Ndipo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa awamu ya nne ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete akaitisha kikao cha kamati kuu ya CCM kujadili kukubaliana kwamba ukumbi wa mikutano wa CCM Chimwaga utumike kama madarasa (lecture theater) ya wanafunzi na ofisi za waalimu. Serikali pia ikaridhia chuo kikuu Dodoma kikaanza Septemba 2007 kwa wanafunzi wa Masters, serikali pia ilikodi floor mbili za NMB Bank Chamwino Branch, mjini pale Nyerere Square. Mwezi Juni 2008 ujenzi ulianza kwa kasi.
Picha ya jengo la ukumbi wa UDOM wakati Ujenzi unaendelea mwaka 1991