Kuanzia Kesho Kila Mwanaume Ampost Mwanamke/Mpenzi Wake - Makonda

Kasomi

JT Founder
Kuanzia Kesho Kila Mwanaume
Ampost Mwanamke/Mpenzi Wake - Makonda

Kutoka kwenye hafla ya michezo ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8, Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda amewataka wanaume kuonyesha hadharani upendo wao kwa wake na wapenzi wao.

"Kila mwanaume kuanzia kesho aposti mpenzi wake au mke wake mitandaoni kuonyesha jinsi anavyomjali na kumpenda," amesema Makonda

Makonda ameeleza kuwa wanawake wamekuwa nguzo muhimu katika jamii na wanastahili kuthaminiwa si kwa maneno tu, bali kwa vitendo. "Wanawake wamekuwa wakituunga mkono kwenye kila hatua ya maisha, ni wakati wetu kuonyesha tunawathamini,"

Tazama video hapa
 

Similar threads

Back
Top